Facebook nao walianzisha Stories kule, lakini cha kushangaza ni kwamba kipengele hicho hakijajipatia umaarufu mkubwa hivyo watu wengi hawakitumii.
Hapa Facebook inafanyia kipengele hiki majaribio, kipengele hiki kitawezesha mtumiaji wa Instagram kuweza ku’share Stories zake moja kwa moja katika mtandao wa Facebook. Hii dhahiri ni njia moja wapo ya kurudisha kipengele cha FB stories kwa kulazimisha.
Vyanzo mbali mbali vya habari havijapendezwa na taarifa hii na wengi wametoa mawazo yao juu ya hili, la muhimu kujua ni kwamba Facebook ni mtandao mkubwa sana na una mambo mengi hivyo ni vigumu kwa mtu kuwaza kuwa kuna stories za kuangalia
Kwa mfano Stories zimekua maarufu Instagram na Snapchat kwa sababu mitandao hiyo haina mambo mengi (picha na video) ndio maana inakuwa ni rahisi kuweza kuona Stories
Facebook kuna mambo mengi sana, kuna habari, magroup, page, status, kungalia video n.k ambapo mambo yote haya yanaweza yakafanyika na kumfanya mtu kutofikiria Stories kabisaaaa!
🚨 ALERT 🚨
Instagram is testing option to share your 'Story' directly to Facebookh/t @mruiandre pic.twitter.com/VTqI92dNJe
— Matt Navarra (@MattNavarra) September 6, 2017
Kwa kuwa hili lipo katika majaribio ngoja tusubiri majibu maana hakuna uhakika kama huduma hii itaanzishwa rasmi au la.