Katika suala zima la biashara za simu janja ama kwa hakika naweza kusema ni “vita” ambayo haijulikani ni lini itafikia ukomo. Sasa Google nao wapo njiani kutambulisha Pixel 2 na Pixel 2 XL.
Baada ya Apple na Samsung kutambulisha simu zao ambazo zinasemekana kuwa gumzo kutokana na mambo kadha wa kadha yaliyomo kwenye simu janja hizo Google nao hawajataka kuwaacha wapenzi wa bidhaa za Google wakisubiri sana kitu ambacho imewaandalia wateja wake na ulimengu mzima kwa ujumla.
Simu janja za Google Pixel ni muendelezo tu simu hizo kutoka familia moja, yaani Pixel ambapo toleo la nyuma yake lilisifika sana kwa kamera yenye ubora na hata kupata tuzo mbalimbali.
Je, ni nini kilichoboreshwa kwenye toleo jipya Google Pixel 2 na Pixel 2 XL?
>Prosesa/Kioo.
SImu zote mbili (Pixel 2 na Pixel 2 XL) zitakuwa na prosesa inayofahamika kama Qualcomm Snapdragon 835. Ukubwa wa kioo kwa Pixel 2 utakuwa ni inchi 5 kilichotengenezwa na HTC (ambapo hivi sasa kampuni ijulikanayo kama HTC imenunuliwa na Google).
>RAM/Diski ujazo
Google Pixel 2 na Pixel 2 XL zote kwa pamoja zina ukubwa GB 4 za RAM huku zikitofautiana kwenye diski ujazo ambao ni kati ya GB 64 mpaka GB 128. Kuna uwezekano wa simu hizo kuja na toleo jipya la programu endeshi (Android 8).
>Sehemu ya kuchomekea “earphones”/USB Type C
Tangu Apple watambulishe teknolojia ya simu yao (iPhone 7) kutokuwa na sehemu ya kuchomekea spika za masikioni kampuni kama Google nao wameona si vibaya wakiitumia teknolojia hiyo kwenye simu janja mbili (Pixel 2 na Pixel 2 XL) lakini simu hizo pia zitakuwa zinatumia teknolojia ambayo pia ni maarufu sana katika miaka ya hivi karibuni, USB Type C. Kujua zaidi kuhusu USB Type C BOFYA HAPA!.
>Bei/Usalama
Goolgle ni moja ya makampuni ambayo bidhaa zake kama simu janja kutokuwa ghali lakini simu janja Pixel 2 na Pixel 2 XL zinatarajia kuuzwa kati ya $849 ya GB 64 (Tsh. 1,910,250) na $949 ya GB 128 (Tsh. 2,135,250). Simu zote za Pixel 2 zitakuwa na ule mfumo wa sensa anbayo ukigusa tu kwa kidole chako basi simu yako inafunguka.
Google wamejipanga kuleta ushindani katika soko la simu janja ambalo mpaka hivi sasa linaonekana kutawaliwa na Samsung Galaxy Note 8 na iPhone 8/iPhone X. Wewe kama mpenzi wa simu janja unazinzunguziaje simu janja mpya kutoka Google?
Vyanzo: The Guardian, The Verge.
2 Comments
Comments are closed.