Ripoti iliyotolewa na KeyBanc Capital Markets inasema kuwa mauzo ya simu za iPhone 8 na iPhone 8 Plus yamedorora kinyume na matoleo mengine ya simu za kampuni ya Apple.
Katika kipindi hiki cha majira ya joto iPhone 8 na iPhone 8 Plus imeonekana kutowapa watu msisimko kama ilivyo kwa simu za matoleo yaliyopita hususani iPhone 7. KeyBanc Capital Markets walikusanya data za utafiti katika maduka ya wauzaji wa simu hizo na ikagundulika kuwa simu za iPhone 7 na iPhone 7 Plus ziliuza haraka kuliko ilivyo sasa kwa iPhone 8 na iPhone 8 Plus.
Mpaka sasa jumla ya simu za iPhone 8 na iPhone 8 Plus zimeuzwa 900,000 katika maduka yaliyofanyiwa utafiti. Mchambuzi John Vinh amegundua kuwa watumiaji wengine wameonyesha nia ya kununua iPhone X ambayo inatarajiwa kuanza kuuzwa Novemba 3 mwaka huu.
Wengi waliohojiwa na shirika la habari la Reuters walisema kwamba iPhone 8 na iPhone 8 Plus hazina jipya kutofautisha sana na iPhone 7 na iPhone 7 Plus hivyo kuwafanya wasubiri toleo la iPhone X.