4G Bado Haijakufurahisha? Tegemea 5G Kutoka Samsung Na LG!

0
Sambaza

Kwanza kabisa fahamu tofauti kuu kati ya teknolojia za 2G, 3G Na 4G kwa Kubofya hapa. Sasa Kutoka katika Blog isiyo rasmi kampuni ya Samsung imeeleza wazi kuwa itaunga majeshi na kampuni ya LG katika kitengo chake cha simu ili kuwezesha teknolojia ya 5G.

Hatua hii itakuza kampuni hizo mbili kwa kiasi kikubwa sana. Ushirikiano huo pia utaongeza uongozi wa korea ya kusini katika utafiti wa teknolojia za 5G. uunganaji huu umekuwa mstarii wa mbele katika uvumbuzi kwa ujumla katika mawasiliano ya simu

SOMA PIA:  Simu zenye 5G kuja mwaka 2019: Fahamu zitatolewa na nani. #Qualcomm

Lg-and-samsung_0

Pia katika swala zima la kukuza teknolojia hii ya 5G litahitaji mjumuiko wa teknolojia mpya ambazo zote zitaletwa na Samsung pamoja na LG katika ushirikiano wao. LG na Samsung wanataka kuwa viongozi katika swala zima la uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali katika swala zima la mawassiliano ya simu

Ushirikiano huu unategemewa kuongeza uwezo wa kasi ya mitandao ya simu kwa kupunguza ucheleweshaji wa data na hata gharama kwa ujumla. Hata hivyo ili makampuni haya mawili yafanikiwe inabidi yafanye kazi mbalimbali kwa pamoja katika ushirikiano wao huo.

SOMA PIA:  Cubimorph: Fikiria kuwa na simu yenye uwezo wa kukunjwa na kupangwa vile upendavyo

Katika Ushirikiano huo na LG ndani ya korea ya kusini pia Samsung wameingia mikataba ya kushikiriana na waendeshaji wengi waliobobea katika masoko ya LTE duniani kote. Hii inajumuisha makubaliano yaliyoingiwa na waendeshaji wa Ulaya, Japan na korea kusini.

Samsung hata hivyo wamekua katika mstari wa mbele katika Mashirika mbalimbali kuhusiana uboreshaji na uendeshaji wa teknolojia ya 5G. hiyo inajumuisha uwepo wa Samsung katika MT-2020 group of the International Telecommunication Union, the World Radiocommunication Conference, the 5G Forum ya Korea ya kusini na the 5G Public Private Partnership ya Ulaya.

SOMA PIA:  Udanganyifu unaoweza kusababisa 'ukaibiwa kidigitali' wabainika kwenye bidhaa za Apple

Licha ya Samsung na LG kushirikiana na kuwa mstari wa mbele tuambie utayari wako wa kuipokea teknolojia hii upo asilimia ngapi? Dondosha lako la moyoni sehemu ya Comment hapo chini.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com