Acer Switch: Laptop za Bei nafuu zinazobadilika na kuwa tableti! #Windows10

0
Sambaza

Ushindani kwa laptop za Chromebooks? Ndivyo inavyoonekana na ujio wa laptop za bei nafuu zinazoweza kuwa tableti zinazotumia OS ya Windows 10 ; Acer Switch One 10 na Acer Switch V 10.

Acer Switch One

Muonekano wa Acer Switch One

Laptop iliyopewa jina la Switch One 10 mpya kabisa itagharimu dola 199 za kimarekani (Takribani Tsh 439,000/= | Ksh 20,000/=) wakati Acer Switch V 10 itamgharimu mtu dola 250 za marekani (Takribani Tsh 548,000/= | Ksh 25,000/=).

Switch V 10 imeboreshwa zaidi na ata bei ni juu kidogo. Ina muonekano bora zaidi (premium) ukilinganisha na Acer Switch One 10.

SOMA PIA:  Kupatikana kwa Ms. Office kwenye Chromebook zote

Kwa hiyo dola 50 zaidi unapata yenye bodi la kuvutia zaidi la chuma (metal) na pia teknolojia ya kuchaji ya kisasa ya USB Type C, kisoma alama za vidole (fingerprint sensor), kioo/display ngumu ya gorilla glass na pia uwezo wa zaidi ya lisaa moja la kukaa na chaji.

 

 

Acer Switch V 10

Muonekano ‘premium’ wa Switch V 10

 

Acer switch

Mikao mbalimbali inayowezekana katika laptop hizi mpya za Acer Switch One 10 na Switch V 10

Sifa kuu;

  • Display – Inchi 10.1,
  • Kioo ni cha mguso (touchscreen) na hivyo unaweza tumia kama tableti
  • Prosesa ya Quad-core Atom
  • Kamera mbili, ya nyuma na ya selfi
  • Uwezo wa kukaa na chaji wa hadi masaa 8 kwa Switch One 10, na masaa 9 kwa Switch V 10
  • Keyboard ya kuchomekwa na kuchomolewa
  • Wembamba wa mm 8.9 na uzito wa kg 1.17
  • Ujazo: GB 32 na GB 64
SOMA PIA:  Programu ya kuokoa data kutoka kwenye simu/kompyuta

Ukilinganisha bei ya laptop hizi zinazoweza kugeuka tableti kwa kweli Acer wameleta ushindani mkubwa kwa laptop za Chromebook na pia kwa ata tableti za iPad kutoka Apple.

Tupe mtazamo wako? Je unazionaje laptop hizi?

Chanzo: Forbes na vyanzo mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com