AdBlock Plus; Huduma ya Kuzuia Matangazo Ishaishinda Facebook

0
Sambaza

Ni siku mbili tatu tuu tokea Facebook watangaze kufanya maboresho ya mfumo wa matangazo kiasi cha kufanya huduma za kuzuia matangazo ya mtandaoni (AdBlock) kutofanikiwa kuzuia matangazo yao…na sasa tayari watengenezaji wa huduma za kuzuia matangazo wameweza kuushinda mfumo wa Facebook.

adblock plus

Facebook wanategemea matengazo kwa kiasi kikubwa katika kukuza mapato yao. Utajiri mkubwa wa kampuni hiyo unatokana na matangazo yaliyo kwenye mtandao huo.

Ukuaji wa watu wengi kutumia huduma za kuzuia matangazo kumefanya Facebook na mitandao mingine inayotegemea mapato kupitia matangazo ya mtandaoni kuathirika. Uboreshwaji wa mfumo wa matangazo wa Facebook dhidi ya apps za kuzuia matangazo ulitegemewa kufanikiwa na ni aibu mfumo huo waliosema wameufanyia kazi kwa muda sasa kushindwa ndani ya masaa 72 tokea kuanza kutumika rasmi.

Inasemakana kuna takribani watumiaji milioni 200 wa kompyuta wanaotumia huduma za kuzuia matangazo, na pia kuna wengine milioni 420 wanaotumia huduma ya kuzuia matangazo kwenye simu janja zao.

Huduma za kuzuia matangazo za AdBlock Plus zinapatikana kupitia ‘extensions’ kwenye vivinjari vya kompyuta kama Chrome na Firefox huku kwenye simu huduma hiyo ikipatikana kupitia app yao.

Facebook nao tayari wameshaboresha TENAA mfumo wao

Masaa machache baada ya AdBlock Plus kutoa toleo lilowashinda Facebook nao Facebook wakatoa taarifa kuhusu suala hilo huku wakidai tayari wanafanya maboresho ya mfumo wao wa matangazo ili kuweza kushinda huduma ya kuzua matangazo ya AdBlock Plus.

matangazo facebook ads

Matangazo ndio chanzo kikubwa cha pesa kwa kampuni ya Facebook

Kwa sasa inaonekana suala hili litakuwa likiendelea kwa muda sana…Facebook watafanya maboresho – AdBlock Plus nao wataleta kitu kipya kuwashinda…na mchezo utaendelea hivyo hivyo… Hahahhaaaa.

SOMA PIA:  Mozilla Yafanya Mabadiliko Katika Logo!

Je unaonaje suala hili la vita dhidi ya matangazo ya kimtandao? Je ni sawa?

Soma taarifa ya kuhusu Facebook na vita dhidi ya huduma za kuzuia matangazo -> Facebook Waboresha mfumo wa Matangazo; ‘AdBlock’ Kuathirika

AdBlock Plus -> Tovuti yao

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com