Adele amkomesha aliyekuwa akimrekodi; Je alikuwa sahihi?

0
Sambaza

Mashabiki wa mwanamuziki nyota Adele walipigwa na butwaa msanii huyo maarufu aliposimamisha ‘shoo’ yake katikati ilikuwapa muda maafisa wa usalama kumzuia shabiki mmoja aliyekuwa akirekodi video ya shoo hiyo.

Adele ambaye aligonga vichwa vya habari duniani kwa kuuza albamu nyingi zaidi mwaka uliopita alikonga nyoyo za mashabiki kote duniani kwa kibao chake cha Hello.

adele

Hata hivyo hapo jana Adele hakutaka mzaha na hati miliki. Alipomuona mwanamke huyo akirekodi video, Adele ambaye alikuwa jukwaani akiwatumbuiza mamia ya mashabiki waliokuwa katika ukumbi huo wa Verona nchini Italia, alisitisha wimbo huo na aakamsihi aache,

SOMA PIA:  Cubimorph: Fikiria kuwa na simu yenye uwezo wa kukunjwa na kupangwa vile upendavyo

”Tafadhali mbona unanirekodi? Kwanini usikae chini na usikilize burudani moja kwa moja? Mimi nipo hapa nawe mbona unanirekodi?” – Alifoka mwanamuziki huyo raia wa Uingereza.

Angalia video iliyomrekodi wakati anamwambia shabiki mwingine aache kumrekodi

Aliongeza kuwa ”Hii sio DVD hii ni moja kwa moja na wewe kuendelea na kunirekodi kunawasumbua wale waliolipia kuja hapa kujiburudisha. Unafahamu kuwa watu wengi wameshindwa hata kuingia hapa kwa hivyo ingekuwa bora zaidi iwapo ungefunganya madude hayo uketi chini raha mstarehe uburudike pasi na kuwazuia mashabiki wenzako”.

SOMA PIA:  VW yajipanga kuhamia katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme

Hili suala limeleta mabishano mengi miongoni mwa watu, je ilikuwa sahihi yeye kumstopisha mtu aliyelipia tiketi kurekodi kumbukumbu hiyo? Au teknolojia ya simu janja zenye nguvu sana zinarahisisha sana watu kurekodi video wanazoweza ata kutengenezea DVD na kuziuza na hivyo kuathiri mapato ya mauzo ya DVD za show na hivyo Adele alikuwa sahihi?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com