Dunia ya leo imekuwa kijiji na kila siku mambo kadha wa kahda yanachapishwa kwenye mitandao mbalimbali lakini kutokana na hilo wenye mamlaka wakatunga sheria ambayo tafsiri yake ikaleta adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao.
Sasa kuna ukweli kwamba si watu wengi ambao wanafahamu makosa ya mtandao kubwa zaidi adhabu ambayo mtu atapewa kulingana na kosa alilotenda baada ya kubainika kuwa umetenda kosa husika. Hizi ndio aina ya makosa ya mtandao pamoja na adhabu zake:
Aina ya kosa la mtandao |
Adhabu ya kosa husika |
Udanganyifu unaohusiana na kompyuta | Faini isiyopungua Tsh. milioni 20 au mara tatu ya thamani ya fedha inayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua miaka 7 au vyote kwa pamoja |
Wizi wa utambulisho wa mtu binafsi mtandaoni | Faini isyopungua Tsh. milioni 5 au mara tatu ya thamani ya faida inayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua miaka 7 au vyote kwa pamoja |
Kutoa taarifa za uongo | Faini isiyopungua Tsh. milioni 5 au kifungo kisichopungua miaka 3/vyote kwa pamoja |
Picha za ngono (kwa watoto, -18) | Faini isiyopuingua Tsh. milioni 50 au mara 3 ya thamani ya faida inayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua miaka 7 au vyote kwa pamoja |
Picha za ngono (kwa wakubwa, 18+) |
|
Unyanyasaji kwa kupitia mtandao |
Faini isiyopungua Tsh. milioni 5/kifungo kisichopungua miaka 3 au vyote kwa pamoja |
Ujumbe unaotuma bila ridhaa |
Faini isiyopungua Tsh. milioni 3 au mara tatu ya thamani ya faida itakayopatikana kinyume cha sheria/kifungo kisichopungua mwaka 1 au vyote kwa pamoja |