Adidas yatengeneza app yao kwa ajili ya kufanya manunuzi ya bidhaa zao mbalimbali - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Adidas yatengeneza app yao kwa ajili ya kufanya manunuzi ya bidhaa zao mbalimbali

0
Sambaza

Unaweza usiamini kwa kampuni kongwe kama Adidas ilikuwa haina app ya kwao wenyewe inayotangaza bidhaa zao au hata kusema mambo kuhusiana wao tofauti na kwenye tovuti au kwenye matangazo ya televisheni.

buy viagra using paypal Suala hilo hivi sasa ni historia kwani baada ya kuwepo kwenye ulingo wa biashara ya vifaa vya michezo kwa miongo mingi lakini sasa imeamua kuja na app ya kwao mahususi kwa ajili ya kuwezesha watu kuweza kununua bidhaa za Adidas kupitia kwenye app yao.

Kwanini app hiyo imeamua kuanza kuwepo hivi sasa na si huko nyuma?

watch Katika bishara yoyote ili ifanye vizuri ni lazima ijitangaze na kwa mujibu wa Adidas ni kwamba uamuzi wa kutoa Adidas app unatokana na sababu na nia ya dhati ya kuhakikisha wanajidhatiti vilivyo upande wa kutangaza bidhaa zao pamoja na mambo mengine kwenye tovuti.

here Adidas app: Moja ya bidhaa unayoweza ukanunua kupitia app ya adidas.

App hiyo haitakuwa tu inatangaza bidhaa za Adidas tu bali mtumiaji ataweza pia kuona habari mbalimbali kuhusu Adidas na washirika wake (James Harden, Lionel Messi na Paul Pogba), video na habari motomoto kuhusu Adidas.

Adidas wanasema kadri unavyozidi kutumia app yao ndio wanakavyozidi kujua ni bidhaa gani unazopenda kwa kutumia akaunti yao ila mipango ya baadae ni kumuwezesha mtumiaji kuweza kuingia kwenye akaunti yake (login) kwa kutumia akaunti ya Runtastic.

Adidas app inapatikana kwenye Android pamoja na iOS. Ni wakati wako sasa wa kuipakua app hiyo kwenye simu yako na kuweza kununua bidhaa za Adidas kwa urahisi zaidi. Unauzungumziaje uamuzi wa Adidas kuwa na app yao yenye kwa ajili ya kufanya manunuzi ya bidhaa zao kupitia Adidas App?

Vyanzo: Engadget, Highsnobiety

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Tetesi: Muonekano wa simu mpya za iPhone
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.