Simu rununu nyingi zina sifa za kuishiwa na umeme baada ya saa chache na nyingine ndani ya dakika kadhaa tu inakuwa imeisha chaji hivyo itakupasa utenge muda ili betri limeweze kupata umeme.
Kutokana na kwamba simu janja nyingi zinakuwa hazikai na chaji kwa muda mrefu ndio maana makampuni mbalimbali yakaona kuna haja ya kubuni teknolojia itakayosaidia watu kuchaji simu zao tofauti na mfumo uliozoeleka.
Neno Power Bank si geni kabisa masikioni pa watu na hasa kwa wanaoyuia simu janja kutokana na ile kasumba ya simu zao kuishiwa na chaji ndani ya muda/saa chache tu baada ya kuichaji.
Belkin Power ni moja ya kampuni ambayo inasifika sana kwa utengenezaji wa vifaa vya kuchaji simu mahali popote pale na hivi karibuni imetoa aina mbili tofati ambavyo vina nguvu kiasi cha 5,000mAh, kingine kina 10,000mAh huku kubwa kabisa ikiwa na 15,000mAh.
Vifaa hivi vyote kwa ujumla wake vina teknolojia ya kuchaji haraka, sio vizito, ile sehemu ya kuchomeka USB (ukubwa wa inchi 6), ina sehemu ya USB ndogo (micro USB) na zote zina taa nne kuonyesha kiasi cha umeme uliopo.
Bulkin Power Bank yenye 5,000mAh|10,000mAh|15,000mAh.
Kwa mujibu wa kampuni iliyoitengeneza wanasema ina uwezo wa kuchaji iPhone 7 mpka ikajaa mara moja na nusu huku ile yenye 10,000mAh ikichaji mara 3 halafu ile kubwa kabisa ya 15,000mAh ina uwezo wa kuchaji mpaka mara 5 ndio uiweke kwenye chaji tena.
Vifaa hivi pia vina uwezo wa kuchaji kamera, sspika za masikioni, spika za kawaida za kuchaji, ndege ndogo zisizokuwa na rubani (drones), kifaa chochote chenye uwezo wa kuchaji kwa njia ya Bluetooth.
Bei zake ni $29|Tsh. 66,700, $39|Tsh. 89,700 na $49|Tsh. 112,700 kuanzia le ile ndogo mpaka kubwa kabisa na upatikaji wake kwa bei hizo ni kwa kuagiza.
Vyanzo: Gadgets 360, TechRadar