Mara kwa mara tumekua tukisikia kuhusu ya makosa ya mtandaoni lakini je, tunayajua? Kumbuka kutotekeleza (kwenda nje na matakwa ya sheria).
Leo nimependa tuangazazie aina za makosa ya kimtandao na ni matumaini yetu kwamba kutokana na makala hii kuna kitu utajifunza. Makosa ya mtandaoni yamegawanyika katika sehemu nne ambazo ambazo ni kama ifuatavyo:-
- Makosa dhidi ya usiri, usalama na upatikanaji wa taarifa za kompyuta/mifumo ya kompyuta hii ikiwa na kuingilia kompyuta au mfumo wa kompyuta (system) kinyume cha sheria, wizi wa taarifa za mtandao.
- Makosa dhidi ya kutumia kompyuta ni pamoja na:
- udanganyifu kwa kutumia kompyuta,
- kugushi kwa kutumia kompyuta,
- wizi wa utambulisho wa mtu binafsi mtandaoni na
- matumizi ya vifaa vya kidujiti kinyume cha sheria.
- Makosa yanayohusiana na maudhui kama vile:
- usambazaji wa picha/picha jongefu za ngono,
- kashfa na taarifa za uongo,
- makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki,
- michezo ya kamari mtandaoni kinyume cha sheria na
- makosa dhidi ya haki na hati miliki
- Sheria inatambua muungano wa makosa kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.