Mkataba wa manunuzi ya ndege 430 kwa dola bilioni 49.5 waweka rekodi! #Airbus #IndigoPartners

0
Sambaza

Kampuni ya ndege ya Airbus ya nchini Ufaransa imepata mkataba mkubwa zaidi kuwahi kupatikana kutoka kwa mnunuaji mmoja wa ndege. Wamepata mkataba wa kutengeneza ndege 430 kwa dola bilioni 49.5 za Kimarekani.

Shirika moja la uwekezaji linalokwenda kwa jina la Indigo Partners la nchini Marekani litalipa pesa hiyo ambayo ni zaidi ya Tsh Trilioni 111.

Mkataba huo utahusisha ndege za familia ya A320neo, ambazo ni ndege za kisasa na zinazosifika sana katika suala la utumiaji wa mafuta – zinakula mafuta machache na huku zikiwa na utendaji mzuri.

Mkataba wa manunuzi ya ndege 430 kwa dola bilioni 49.5 waweka rekodi

Mkataba wa manunuzi ya ndege 430 kwa dola bilioni 49.5 waweka rekodi!

Oda hii imeweka rekodi: Ndio oda ya ndege nyingi zaidi kuwahi kuwekwa na mnunuaji mmoja.

Shirika la Indigo Partners linamiliki asilimia flani katika mashirika ya ndege ya Volaris Airlines (nchini Mexico) na Wizz Air (Nchini Hungry). N pia shirika linaumiliki mzima katika mashirika ya ndege ya Frontier Airlines (nchini Marekani) na JetSMART Airlines (nchini Chile).

airbus A320neo

Airbus A320neo

Mgawanyo wa ndege hizo, 273 zitakuwa za A320neos na 157 zitakuwa jamii ya A321neos;

  • Wizz Air: 72 za A320neo na 74 za A321neo;
  • Frontier Airlines: 100 za A320neo na 34 za A321neo;
  • JetSMART: 56 za A320neo na 14 za A321neo;
  • Volaris: 46 za A320neo na 34 za A321neo.
SOMA PIA:  Shirika la ndege la Uingereza lakumbwa na tatizo la kompyuta.

Ndege hizo zitaingizwa katika mashirika hayo, uamuzi wa kuweka oda moja unasaidia kushusha gharama.

Kwa kipindi chote cha mwaka huu shirika la utengenezaji ndege la Boeing ndilo lilikuwa linaongoza kwa kiasi kikubwa katika mauzo na hivyo mkataba huu unawaweka Airbus katika eneo nzuri kwenye ushindani – hali isipobadilika inaweza wafanya kuwa namba moja kwa oda za ndege kwa mwaka huu.

Mkataba (MoU) kati ya Indigo Partners na Airbus umefanyika katika maonesho ya kimataifa ya ndege yanayoendelea huko Dubai.

Vyanzo: CAPA na tovuti mbalimbali

SOMA PIA:  Matumizi ya simu janja pamoja na 'Drones' katika kupambana na Malaria

(Masahihisho: Mwanzo tulikosea na kuandika Airbus ni ya nchini Marekani, Boeing ndiyo ya nchini Marekani)

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com