Airbus kufanya majaribio ya magari yanayopaa mwaka huu

0
Sambaza

Magari yanayopaa ni kitu ambacho kina uwezekano mkubwa wa kuwa cha ukweli na si kwenye filamu tuu mwaka huu.

Kampuni nguli katika teknolojia za ndege ya Airbus imesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wanategemea kuwa na gari la kwanza duniani lenye uwezo wa kupaa na kulifanyia majaribio.

airbus magari yanayopaa

Inategemewa magari hayo kusaidia pia watu kusafiri ata maeneo yasiyofikiwa na barabara.

Mchakato wa utengenezaji wa gari hilo uliaanza mapema mwaka jana – Februari 2016. Ubunifu wa gari hilo ulikamilika mwezi wa nane mwaka jana na mara moja waandisi (engineers) wa kampuni hiyo wakaanza kazi ya utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya gari hilo.

SOMA PIA:  Facebook kufundishwa kama kipengele katika somo la Kiingereza nchini India

Litafanyaje kazi?

Inategemewa likiwa barabarani litafanya kazi kama gari jingine lolote ila kwa kubonyezwa tuu sehemu flani kutakuwa na mabadiliko yatakayoliwezesha gari hilo kuweza kupaa na kuendeshwa hewani.

Inategemewa miji itaendelea kukua kwa kasi na hivyo foleni za barabarani ni janga ambalo halitaweza kuepukwa ila kwa ujio wa magari haya wenye haraka wanawaza fanya maamuzi haraka ya kutumia anga badala ya barabara.

Lengo la Airbus ni pamoja na magari haya kutumika kwa huduma za taksi, kwa usafiri wa haraka kama vile huduma ya Uber inavyofanya kazi.

SOMA PIA:  Makampuni 10 Yanayoongoza Kupata Maombi Ya Kazi Kupitia LinkedIn! #Teknolojia

Ili kuepusha uchafuzi wa hali ya hewa mkurugenzi wa Airbus Bwana Tom Enders amesema ni lazima magari yanayopaa kutumia nishati rafiki kwa mazingira.

Tutaendelea kufuatilia maendeleo yao katika utengenezaji wa gari hili.

Tuambie wewe una maoni gani juu ya utengenezaji wa magari yenye uwezo wa kupaa?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Vyanzo: ZDnet na vyanzo mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com