AirDrop ni nini? Ifahamu njia ya kutuma mafaili kwa haraka kwa watumiaji wa iOS na MacOS

0
Sambaza

AirDrop ni teknolojia ya kitofauti inayopatikana kwa watumiaji wa vifaa vya Apple kama vile iPhone, iPad, iPod na Macs.

Kupitia teknolojia ya AirDrop, basi watumiaji wa vifaa hivyo wanaweza kutumiana mafaili na data kwa haraka zaidi kulinganisha na njia zingine zozote za bila kutumia waya zinazopatikana kwa watumiaji wa vifaa vingine.

airdrop ni nini

Ingawa teknolojia hii ipo katika vifaa vingi vinavyotengenezwa na Apple ila bado ni watumiaji wengi wa vifaa kutoka kampuni hivyo kama vile simu za iPhone na kompyuta za Mac bado hawaifahamu na kama wamekwishaisikia basi bado hawajaona umuhimu wake.

Teknolojia ya AirDrop inawawezesha watumiaji wa bidhaa za Apple kama vile iPhone na Macs kutumiana mafaili ya namna mbalimbali; kama vile, anuani za mitandao (bookmarks), picha, video, anuani (contacts) na data nyingine nyingi.

airdrop

Ufanyaji kazi wa teknolojia ya AirDrop unatumia teknolojia ya Bluetooth na WiFi kwa wakati mmoja.

Je, teknolojia ya AirDrop inafanyaje kazi?

Teknolojia ya AirDrop inatumia teknolojia ya Bluetooth, ila si bluetooth kikawaida ila ni kwamba kwa kutumia teknolojia ya Bluetooth vifaa viwili vya Apple vinafanikiwa kutengeneza mawasiliano kupitia teknolojia ya WiFi inayokuwa spesheli kwa vifaa hivyo viwili tuu.

SOMA PIA:  Mambo 8 ambayo si rahisi kujua kwenye simu za Samsung Galaxy

Data kutoka kifaa kimoja kwenda kingine zinakuwa zipo chini ya hatua za kiusalama za juu kiasi ya kwamba inakuwa ni salama zaidi kutuma data kupitia AirDrop kuliko hata kutumia njia za kawaida za kimtandao.

airdrop

Utumwaji wa faili

Je, kwa nini njia za kutumiana mafaili za Android zinakuwa bado nyuma kulinganisha na hii ya AirDrop?….wakati zote zina teknolojia ya Bluetooth?

Tofauti kuu ni kwamba kwa Android bado utumaji wa mafaili unatumia teknolojia ya bluetooth kama ilivyo na pia kuna vifaa vinayvochanganya teknolojia hii pamoja na teknolojia ya NFC kwa wakati mmoja ila bado teknolojia hizo haziifikii teknolojia ya hii.

SOMA PIA:  Ulinzi madhubuti wa kudhibiti barua pepe kudukuliwa (mtu mwingine kuitumia)

Utofauti ni kwamba ingawa AirDrop inaitaji teknolojia ya Bluetooth kufanya kazi ni kwamba inatumia teknolojia hiyo kutengeneza mawasiliano ya mfumo wa WiFi, na hivyo mafaili hutumwa kupitia mfumo wa WiFi na si bluetooth. Na hii ndio maana mafaili hata kama ni ya ukubwa zaidi (GB 1 na hata zaidi) yanaenda kwa kasi zaidi. – Kumbuka utumiaji huu wa teknolojia ya WiFi hauusishi huduma ya intaneti KABISAAAA.

Kwa vifaa kama vile iPhone na iPad teknolojia hii inaweza kutumika kwa vifaa vinavyotumia toleo la iOS 7 wakati kwa Macs ni kuanzia toleo la Mac OS X Lion (10.7).

Soma – Jinsi Ya Ku Share Mafaili Kati Ya iPhone, iPad na Mac Kupitia AirDrop! 

Je, umeshawahi kutumia au kusikia kuhusu teknolojia hii? Tuambie unaionaje.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com