Airplane Mode ni nini? Fahamu matumizi na faida zake! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Airplane Mode ni nini? Fahamu matumizi na faida zake!

0
Sambaza

Mfumo wa Airplane Mode unapatikana kwenye vifaa vingi vya elektroniki kama vile simu janja na ata tableti. Je ushawahi jiuliza ni nini hasa matumizi yake?

android notifications airplane mode ni nini

Kwa asili yake ni teknolojia iliyowekwa kwenye vifaa vya elektroniki kuepusha muingiliano wa mawasiliano kama vifaa hivyo vikitumika kwenye sehemu kama vile ndege na sehemu yeyote ambayo haiitajiki muingiliano wa vyombo vya mawasiliano.

purchase Finax canada Simu au tableti yako ikiwekwa kwenye mfumo wa Airplane Mode utaweza kugundua kupitia kialama cha ndege ilukayo kinachokuwepo katika eneo la ‘Notifications’.

go to link Airplane Mode inasaidia kuzima teknolojia ya mawasiliano ya – kiredio (mjumuisho wa Bluetooth, WiFi na mitandao ya simu) kwa njia rahisi ya kuchagua eneo moja tuu.

Kitendo cha kuweka Airplane mode kitasaidia ata kufanya simu au tableti yako kudumu muda mrefu zaidi na chaji ingawa hili litafanikiwa kutokana na huduma nyingi kuzimwa.

INAYOHUSIANA  TTCL na vifurushi vya usiku

>Celullar: Mfumo wa mawasiliano ya simu kupitia laini yako huzimwa.

Hii inamaanisha huduma za kupiga na kupokea simu, ujumbe wa SMS na huduma ya intaneti (data) kupitia mtandao wako wa simu huzimwa pia.

>WiFi huzimwa pia.

Huduma ya intaneti kupitia mfumo wa WiFi huzimwa pia. Ingawa kwa baadhi ya vifaa vya kisasa zaidi bado unaweza kuwasha huduma ya WiFi baada ya kuweka Airplane Mode.

>Bluetooth

Utumiaji wa Airplane Mode huzima pia huduma za bluetooth.

>GPS huzimwa pia

GPS ni moja ya teknolojia muhimu kwa simu za kisasa inayotumiwa na apps nyingi kuweza kutambua masuala ya kijiografia kuweza kutambua kifaa chako kipo eneo gani duniani.

Je kuna faida gani ya kutumia Airplane Mode?

airplane mode

Chaguo la Airplane Mode katika simu za iPhone na tableti za iPad

Kwenye baadhi ya maeneo hakuna ruhusa ya watu kuweza kutumia vifaa vya mawasiliano vinavyoweza kuingiliana na mfumo mwingine wa kimawasiliano, mfano kwenye ndege.

INAYOHUSIANA  Simu mpya ya Oppo Find X yazinduliwa Ufaransa

Teknolojia hii imerahisisha watu wenye vifaa vya elektroniki kuweza kuvitumia ata pale wakiwa kwenye ndege kama tuu wakihakikisha vifaa hivyo vimewekwa kwenye Airplane Mode.

Inasemekana muda wote simu zinatuma signal kutafuta mnara wa mawasiliano na kama ndege yenye abiria wengi ndani yake na wote wakiacha simu zao zikiwa zimewaka basi itapokuwa hewani simu hizo zote zitakuwa zinatuma signal nyingi za kutafuta mawasiliano na hili linaweza ingiliana na mfumo wa mawasiliano wa ndege na hili linaweza leta tatizo kwa rubani katika ufanisi wake.

http://marylydon.com/san-diego-architecture-and-design-shows-who-we-are/?s= Pia faida kuu inaweza ikawa kwenye kukusaidia kuendelea kutumia kifaa chako kwa kazi zingine bila utumiaji mwingi wa chaji. Hii ni kwenye simu, tableti na ata baadhi ya laptop.

INAYOHUSIANA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

Kumbuka mara zote kifaa chako kinapokuwa kimeweka basi kuna mifumo mingi ya kimawasiliano ya kiredio – yaani mtandao wa simu, bluetooth, wifi na GPS huwa vinafanya kazi inayotumia kiwango kikubwa cha chaji.

Baadhi ya vifaa vinaruhusu WiFi na Bluetooth kufanya kazi ata vikiwa kwenye Airplane Mode.

Huduma ya WiFi ikitumika wakati simu nzima ipo katika mfumo wa Airplane mode

Baadhi ya vifaa vya kisasa zaidi vinaruhusu baada ya kuweka kifaa chako kwenye Airplane Mode utaweza kuwasha na kutumia huduma za WiFi au Bluetooth.

Hii ni kwa sababu kwa siku hizi kuna hadi ndege zinazotoa huduma ya WiFi ndani yake, zina teknolojia kubwa ya kusaidia kuepusha teknolojia hiyo kuingiliana na teknolojia za kimawasiliano za ndege.

Je huwa unaitumia teknolojia ya Airplane Mode? Na katika hali gani unajikuta unatumia teknolojia hii?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.