Airtel Waondoa Bando la GB 1/Siku, Washambuliwa Twitter - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Airtel Waondoa Bando la GB 1/Siku, Washambuliwa Twitter

0
Sambaza

Labda wenyewe wamejipanga vizuri….au labda wamefanya makosa na muda si mrefu uamuzi huu utawang’ata wenyewe. Katika hali ya kitofauti Airtel waondoa bando la GB 1 kwa siku na kufanya kifurushi cha MB 400/kwa Siku kuwa Tsh 1000.

Soma Pia –  http://artonthewaterfront.ca/project/lizzielin-designs/ TCRA: Ubora wa huduma kwa mitandao ya simu Tanzania!

airtel waondoa bando

Ushindani ni mkubwa kwa muda huu kuliko kipindi kingine chochote katika mitandao ya simu. Kuja kwa Halotel, mtandao uliowekeza zaidi kwenye huduma ya intaneti ya kiwango cha 3G kumeleta ushindani mkubwa kwa mitandao mingine yote – Airtel, Tigo, Zantel.

http://moonraceranimalrescue.com/meet-stella/ Kwa muda huu kila mtandao unajaribu kuja na kitu cha kuwavutia zaidi wengine, na kwa kweli ni jambo la kushangaza kuona Airtel wanachukua uamuzi ambao unaweza kuwaathiri zaidi. 

Kufikia mwezi wa nne mwaka huu tayari data kutoka TCRA zilikuwa zinaonesha nafasi ya pili kwa namba ya wateja iliyokuwa inashikiliwa kwa muda mrefu na Airtel tayari inaonekana kuchukuliwa na Tigo. Ukijumlisha ukuaji wa haraka wa Halotel na ukuaji mkubwa wa ushindani si muda mrefu tutasikia Airtel ipo katika matatizo.

INAYOHUSIANA  Tanzania: Inashika nafasi ya 149 kwa kasi ya intaneti

click Uamuzi kama huu unaonekana umekaa kimapato zaidi na hivyo inaweza ikawa inaashiria ya kwamba kama wakiweka bei za ushindani za sasa basi watakua wanapata hasara kiuendeshaji…na kama ni hivyo basi wapo kwenye hali mbaya kibiashara…

NINI KITAFUATA?

Screen Shot 2016-08-11 at 10.57.02 AM airtel tigo

Watanzania wengi wanatumia laini zaidi ya moja, na pia hawaogopi kujaribu mtandao mwengine mpya kwao. Kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii – Facebook, Twitter, WhatsApp na kuperuzi sana kwa siku basi uamuzi huu hakika utawafanya wahamie upande wa pili. NA HILI LITAWAUMIZA AIRTEL MUDA SI MREFU.

Soma Pia – TCRA: Ubora wa huduma kwa mitandao ya simu Tanzania!

INAYOHUSIANA  Airtel Tanzania yajiunga mfumo wa malipo kwa GePG

Je wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Airtel? Tuambie kama mabadiliko haya yamekuathiri tayari?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.