Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Airtel imekanusha madai kwamba inaondoka nchini Kenya kutokana na hali ngumu ya kibiashara, imeripotiwa.
Kampuni hiyo imekanusha madai hayo baada ya baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kueneza habari hiyo Jumatatu jioni.
Airtel ilisema licha ya kusema kuwa ilikuwa tayari kuungana na kampuni nyingine au kununuliwa hasa sehemu ambazo hazifanyi vyema, Afrika, ikiwemo ni pamoja na Kenya.
Kulingana na taarifa ya Airtel Africa, ilikuwa ikitathmini njia zingine kwa lengo la kuimarisha biashara na mapato yake. “Hatukusema tunaondoka katika soko la Kenya, tulisema tunatafuta njia za kuimarisha biashara,” Airtel ilisema katika taarifa.