Aishtaki Apple, Asema Imeiba Ubunifu Wake Na Inabidi Imlipe Dola Bilioni 10 Kama Fidia!

0
Sambaza

Kampuni ya Apple kwa sasa inatuhumiwa na mwanaume mmoja kutoka Florida, ambae analalama kuwa kampuni hiyo imemuibia ubunifu wake wa mwaka 1992

Jamaa huyo anasema ubunifu wake huo ndio umepelekea mpaka Apple wakatengeneza simu za iPhone, iPod na iPad. Kwa kifupi ni kwamba jamaa anadai ameibiwa ubunifu huo tena ukiwa katika Mchoro (michoro)

Mchoro Huo Ukiwa Na Baadhi Ya Maelezo

Mchoro Huo Ukiwa Na Baadhi Ya Maelezo

Jamaa huyo anaejulikana kama Thomas S. Ross anaomba alipwe fidia ya bilioni 10 za kimarekani na kampuni hiyo (Apple) – pesa hizo ni nyingi sana – kidogo hii inaweza ikawa inawashangaza wengi, lakini kwa namna moja au nyingine kesi hii ipo!

SOMA PIA:  China yawasha mtambo wa umeme wa nguvu za jua unaoelea ziwani

Thomas alikiambia kituo cha Guardian kuwa anajua anapigana vita kubwa sana kwani analishtaki moja kati ya kampuni kubwa kuliko yote duniani na katika vita hiyo yuko yeye peke yake, lakini hataishia hapo kwani haki ni haki tuu!

“Sikuweza kuuifikisha ubunifu wangu mbali zaidi kwani nilikuwa masikini, mpaka sasa bado ni masikini. Na pia sikuwa mzuri katika kuwafuata wawekezaji na kuwauzia mawazo yangu” – Alisema Thomas

Michoro ambayo Thomas aliichora ni ya kifaa cha kumuwezesha mtu kusoma au kuchora, maarufu kama ERD (Electronic Reading Device). Thomas anadai kifaa hicho ni chanzo cha kutengenezwa kwa iPhone, iPod na iPad.

ERD Ya Kushuto, Jaribu Kuifananisha Na iPhone Ya Kulia

ERD Ya Kushuto, Jaribu Kuifananisha Na iPhone Ya Kulia

Kumbuka iPhone ndio simu ya kwanza kuja bila ya kuwa na keyboard ya kutachi (zingine zilikuwa na ile ya kubonyeza)

SOMA PIA:  Snapchat Kuleta 'Link' Na 'Background' Katika Stories!

Thomas kwa upande wake anasema mwaka 1992 ambapo aliandaa ubunifu huo na kuuhifadhi kwa njia ya michoro hakuweza kuulipia ili kuusajili uonekane wakwake kwani hakuwa na pesa kipindi hicho. Hali hiyo ilipoendelea kitengo cha marekani cha ubunifu na hakimiliki kiliamua kuachana (kwani haukulipiwa ili uwe unamilikiwa na mtu mmoja) na ubunifu huo.

Mchoro Huo Ukiwa Na Baadhi Ya Maelezo

Mchoro Huo Ukiwa Na Baadhi Ya Maelezo

Kingine cha kushangaza kutoka kwa Bw. Thomas ni kwamba hataki kuishia katika kuomba fidia ya bilioni 10 za kimarekani bali pia amesema kuwa anataka inabidi awe analipwa aslimia 1.5 (1.5%) katika thamani ya mauzo ya iPhone yanayokuja

SOMA PIA:  FAHAMU: Mega Pixel (MP) Ni Nini Na Inafanya Nini Katika Picha!

Kwa sasa kampuni la Apple linaingia mapato ya bilioni 3.5 kwa mwaka, sasa hapo pata picha jamaa akiwa anachukua asilimia 1.5 tuu.

Niandikie sehemu ya comment hapo chini je michoro hiyo inafanana na kifaa chochote kutoka katika kampuni ya Apple? Ningependa kusika kutokia kwako

Pia Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona, ili kuhakikisha unakua karibu na kesi hii, Je jamaa atashinda? Kaa nasi. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com