Ajali ya Kwanza (kuhusisha Majeruhi) kwa Magari Yajiendeshayo ya Google - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Ajali ya Kwanza (kuhusisha Majeruhi) kwa Magari Yajiendeshayo ya Google

0
Sambaza

Kwa mara ya kwanza Google wamerekodi ajali iliyo sababisha majeraha kwa abiria katika moja ya magari yake yanayojiendesha toka mwaka 2009, hii itakuwa ni ajali ya kumi na nne tokea mradi huu wa Google wa magari yanayojiendesha yenyewe unazishwe.

Google-Self-Driving-Car-Logo-medium-001-e1401280599651

Gari hilo aina ya Lexus iliyofungwa kamera za teknolojia ya hali ya juu lilipata ajali hiyo eneo la Mountain view Calfonia Marekani, Dereva wa gari iliyokuwa nyuma aliligonga gari hili lilokuwa limewabeba wafanyakazi wa Google baada yakutokuwa makini.

Wafanyakazi hao wa Google pamoja na dereva wa gari lililowagonga walipelekwa hospitali ya jirani ambako walitibiwa majeraha madogo na baadaye kuruhusiwa, hii ni mara ya kumi na moja kwa gari la Google linalojiendesha kugongwa kwa nyuma.

INAYOHUSIANA  Google Classroom yaboreshwa

Google500KmilesLexus

source Magari haya 25 ya Google hadi sasa yameshasafiri umbali wa zaidi ya kilomita milioni moja  na nusu ndani ya kipindi cha miaka sita, inatarajiwa ifikapo mwaka 2020 magari haya yanayojiendesha yenyewe yatakuwa yanapatikana kwa uma.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply