Akaunti kumi zenye Followers wengi zaidi Instagram 2016 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Akaunti kumi zenye Followers wengi zaidi Instagram 2016

0
Sambaza

Instagram imetoa orodha ya akaunti kumi ambazo zinawafuasi ama followers wengi zaidi kwa mwaka 2016, pamoja na kuwa na watumiaji wengi lakini Tanzania haina mtumiaji hata mmoja ambaye ameweza kuingia katika orodha hii.

source

Wanawake ndio wametawala zaidi orodha hii na wamechukua nafasi nane nafasi mbili tu ndio zimeenda kwa watumiaji wa kiume.

10. Kendall Jenner.

http://animalsinthehaus.com/news/ Nafasi ya kumi imeshikiliwa na mwanamitindo kutoka Marekani ambaye ni mdogo wake na Kim kardashian ameshika namba kumi katika orodha hii huku akiwa na followers wapatao milion 68.9.

9. Nicki Minaj.

see Star na mwanamuziki Nicki Minaji kutoka Marekani aliyevuma katika anga ya muziki na albamu ya Pink friday mwaka 2010 ameshikilia namba 9 katika orodha ya watu wenye  wafuasi wengi zaidi mwaka 2016.

Nicki anawafuasi ama followers milioni 69.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi inawezekana

8. Dwayne Johnson.

Katika nafasi ya nane anasimama Muigazaji na Mcheza mieleka (katika mieleka anajulikana kama The Rock) ambaye anashika nafasi ya nane katika orodha hiyo na wafuasi milioni 71.

dwayne-johnson-12a

7.Kylie Jenner.

Katika nafasi hii yupo binti wa miaka 19 Kylie Jenner ambaye anatokea katika familia ya Kardishian, binti huyu ni star wa televisheni na pia ni mwanamitindo na anawafuasi milioni 79.5 katika mtandao huu wa Instagram.

6. Christiano Ronaldo.

Mwanasoka wa timu ya taifa Ureno pamoja na timu ya Real Madrid ndiye mwanaume wa pili na mwanasoka pekee katika orodha ya watumiaji wenye wafuasi wengi katika mtandao huu. Ronaldo anawafuasi wapatao milioni 82.3

5. Kim Kardashian.

Kim Kardashian ni mwanamitindo na star wa Televishen ambaye pia ni mke wa Kanye West, mwanafamilia huyu wa Kardashian anajiunga na wadogo zake wengine wawili ambao wapo katika orodha hii. Kim ana wafuasi wapatao milioni 87.8.

INAYOHUSIANA  Kodi kwenye mitandao ya kijamii yaanza rasmi Uganda

4. Beyoncé.

Beyoncé Giselle Knowles-Carter ambaye ni mwanamziki wa Marekani na pia ni mke wa mwanamziki Jay Z, mwanamama huyu anasifika kwa kuwa na mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii na katika orodha hii anasimama katika namba 4  akiwa na wafuasi wapatao milioni 88.9 katika mtandao huu.

3.Ariana Grande.

Mwanamuziki kutoka Marekani ambaye tayari amekwisha tamba na vibao kadhaa katika anga za muziki anashikilia nafasi ya tatu akiwa na wafuasi milioni 89.6

2.Taylor Swift.

Nafasi ya pili inashikiriwa na msanii ambaye pia ana mashabiki wengi saana katika mitandao, Taylor ameshawahi kuongoza kwa kuwa na wafuasi wengi katika mtandao wa Twitter.

swift

Taylor ana wafuasi 93.6 milioni.

INAYOHUSIANA  Smile Telecom ya Uganda yawalipia wateja wake kodi ya mitandao kwa miezi mitatu

1.Selena Gomez.

Mwanamuziki na Muigizaji Selena Gomez ameibuka kinara katika orodha ya watumiaji wa instagram ambapo ana wafuasi 103 milioni. Selena alipata umaarufu katika majukumu yake ya uigizaji akiwa binti mdogo lakini pia uhusiano wake na mwanamuziki Justin Beiber ulimpa kiki na wafuasi zaidi.

selena_gomez<_walmart_soundcheck_concert

Sio tu mastaa wa bongo hawamo katika orodha hii bali hakuna staa yeyote kutoka Afrika ambaye alifanikiwa kuingia katika orodha hii pengine hii itakuwa ni changamoto kwa wasanii wetu kujitahidi kuwafikia mashabiki wengi zaidi katika mitandao ambao watawaongezea soko na kuwasaidia kupata mikataba ya matangazo kutoka katika makampuni.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.