fbpx

Alcatel 1X: Simu janja ya kwanza kutumia Android Go

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mwishoni mwa mwezi uliopita Google katika mkutano mkubwa MWC 2018 ilipozindua rasmi mfumo wa Android Go, simu janja ya kwanza kutumia mfumo huo imekuwa Alcatel 1X.

Alcatel 1X nayo imezinduliwa rasmi katika mkutano wa MWC 2018 ikiwa na Android Oreo (Go Edition).
Simu hii ya kiwango cha chini itakuwa na ukubwa wa kioo cha 5.3-inch (960×480 18:9 display).

Pia itatumia Prosesa ya Quad-core MediaTek na ukubwa wa RAM utakuwa ni 1GB na ukubwa wa uhifadhi
ni 16GB.

Alcatel 1X

Alcatel 1X

Kwa upande wa kamera ni kwamba ya nyuma itakuwa na 8MP na ya mbele (Selfie) ina 2MP.
Ujazo wake Betri ni 2,460mAh.

INAYOHUSIANA  Programu tumishi 46 zaondolewa kwenye Google Playstore

Simu janja hii itaanza kuuzwa mwezi April na matarajio ya bei yake ni kutokuzidi dola 100.

Mbali na Alcatel 1X simu zingine zitakazokuwa na Android Go ni Nokia 1, GM 8 Go, LAVA Z50 na ZTE Tempo Go ambazo nazo zilizinduliwa Kwenye MWC 2018.

Nokia 1 , android go

Nokia 1

ZTE tempo Go

ZTE tempo Go

Tutarajie simu nyingi za bei rahisi zinazotumia Android Go kutoka mfululizo. Na hii ni habari njema kwa wale wasiohitaji simu kubwa na ghari.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.