Alibaba watambulisha Gari janja lililounganishwa na intaneti na OS

0
Sambaza

Kuna simu, tableti, kompyuta, mswaki janja n.k, sasa kutana na gari janja linalotaka ulichukulie kama vile ‘gadget’ nyingine yeyote mfano simu.

Soma pia – Mswaki janja wa Tsh Milioni 1, wenye kamera ya HD

Gari hili kutoka kampuni kubwa ya nchini China ya Alibaba ni kama gari jingine lolote ila tu tofauti yake ni kwamba limeunganishwa na huduma ya intaneti na kupitia programu endeshaji (OS) ya YunOS kutoka Alibaba itakusaidia kufanya kazi mbalimbali ambazo ungeweza fanya kwa kutumia simu yako.

Alibaba watambulisha Gari janja

Alibaba watambulisha Gari janja: Ni gari lenye intaneti au ni gari linalotumia intaneti?

“Tunachotengeneza ni si ‘intaneti kwenye gari’ ila ni ‘gari juu ya intaneti'” – Alisema bwana Dr Wang Jian, mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya Teknolojia katika kampuni ya Alibaba

SOMA PIA:  Simu ya LG G6: LG waonesha bado wapo makini na biashara ya simu

Mambo yanayowezekana kutokana na teknolojia ya gari hilo;

  • Ukiweka mafuta sheli na inaitajika kufanya malipo basi gari lenyewe litafanya malipo hayo moja kwa moja bila kuhusisha wewe kutoa kadi au kulipa kwa kutumia simu au app. Gari litatambua kiwango cha mafuta yaliyowekwa na kisha kufanya malipo hayo.
  • Upo njiani na unakaribia kufika nyumbani? – Gari litatuma ujumbe kuhakikisha AC yako ya nyumbani  inawaka na kuweka hali ya hewa sawa kabla ya kufika kwako – (au kifaa chako kingine chochote kilichonyumbani kilichounganishwa na huduma ya intaneti)

Hii ni mifano tuu ila vingi vitawezekana kufanyika kutokana na utumiaji wa apps na huduma ya intaneti vinavyounganishwa katika gari hilo kupitia programu endeshaji yake ya YunOS.

SOMA PIA:  Facebook kufundishwa kama kipengele katika somo la Kiingereza nchini India

(YunOS – ni programu endeshaji inayotengenezwa na Alibaba kwa kutumia toleo huru la Android)

Muonekano wa ndani ya gari hilo

Programu endeshaji ya YunOS iliyokwenye gari hilo imepewa nguvu nyingi hii ikiwa ni pamoja na;

  • Kuweza kumtambua dereva wa gari
  • Vioo (display) vitatu vya kutumika – apps n.k
  • Uwezo wa kupata ramani na uwezo wa kuitumia ata bila huduma ya WiFi au teknolojia ya GPS kuweza kukupeleka unapotaka.
  • Voice Commands – utaweza kuamrisha mambo mbalimbali kwa sauti
  • Kamera nne ndani ya gari hilo zinazoweza kukupa selfi za nyuzi 360… 🙂

Katika video fupi iliyowekwa kwenye mtandao wa Twitter inaonesha vitu vingine vingi vinaweza unganishwa kupitia WiFi ya gari hilo na hivyo gari kuweza kuvi-control, mfano vindege vya Drones.

Teknolojia ya gari hiyo pia imetengenezwa kwenye mfumo wa uwazi – yaani makampuni mengine yanaweza kutengeneza vifaa na apps zenye uwezo wa kutumika kwenye magari haya.

SOMA PIA:  Namna ya kurudisha picha/video ulizovifuta kwenye simu za Android/iOS #Maujanja

Upatikanaji?

Gari hili litaanza kupatikana rasmi kwa ajili ya wateja mwezi wa nane mwaka huu, na hadi sasa mtu unaweza kuweka oda.

Bei?

Bei inategemewa kuwa kati ya dola 14,941 hadi 27,966 za kimarekani (Kati ya Tsh 32,767,854/= – Tsh 61,333,632/= | Ksh 1,511,947 – Ksh 2,830,005/=.. bei itategemea mambo mbalimbali yatakayopendwa na mteja.

Unalionaje hili? China wanazidi kwenda mbele kiteknolojia!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com