Alphabet yapeleka WiFi Puerto Rico kwa mfumo wa maputo yanayopaa

1
Sambaza

Intaneti ni kiungo muhimu sana katika kufanikisha mawasiliano duniani kote na hivyo kuifanya kampuni mama, Alphabet inayomiliki Google, HTC, n.k kuamua kupekeka huduma ya intaneti Puerto Rico iliyokuwa na mafuriko/kimbunga hivi karibuni.

Matumaini ya watu wanaoishi Puerto Rico kuweza kuwasiliana na jamaa zao yamerejea baada ya kampuni nguli kwenye masuala ya teknolojia (ingawa si maarufu kwa wengi 😆 😆 ) kuamua kuwezesha wananchi hao kupata huduma ya intaneti ingawa si kwa njia waliyoizoea.

Tukio hilo la kutoa huduma ya linafamika kama Project Loon ambayo kazi yake ni kuhakikisha watu wa eneo la Puerto Rico wanapata huduma ya intaneti ya uhakika kwa njia ya Wi-Fi inayosambazwa na maputo ya kujazwa upepo na kisha kuelea angani.

Alphabet yapeleka WiFi Puerto Rico

Alphabet yapeleka WiFi Puerto Rico: Project Loon inavyotoa huduma ya intaneti kwa wananchi wa Puerto Rico.

Mafuriko yaliyotokea huko Puerto Rico yameharibu 90% ya minara ambayo ilikuwa ikitoa huduma ya intaneti kwa wananchi wa eneo hilo hivyo kutokana na maafa hayo Alphabet imekuwa nchi ya kwanza kupeleka msaada wao huku Facebook ikisema itapeleka timu ya kwenda kuhakikisha watu wa eneo hilo wanaweza kuwasiliana na ndugu na jamaa zao.

SOMA PIA:  Google Inaweza Ikabadilisha Muonekano Wake Katika Simu Janja!

Changamoto inazokumbananazo Project Loon.

Kile jambo lina changamoto zake kuweza kulifanikisha na ukweli ni kwamba Project Loon si mara ya kwanza kwa Alphabet kutoa huduma hiyo, Brazil na Zealand ni nchi mojawapo ya nchi zilizowahi kufaidika na huduma kama hiyo ilianza kutolewa tangu mwaka 2011.

Haiaminiki iwapo Project Loon itaweza kutoa huduma hiyo ya intaneti katika eneo lote la kisiwani kwani nguvu zaidi za kifedha zinahitaji kuweza kufanikisha watu wa eneo hilo wanaweza kuwasiliana pamoja na mambo mengine. Mbali na Facebook kuahidi kutoa huduma ya intaneti kwa watu wa Puerto Rico pia imetoa msaada wa $1.5M|zaidi ya Tsh. 3,373bn.

Serikali ya Marekani iliahidi kupeleka msaada kwa watu wa Puerto Rico ingawa mpaka sasa bado haijapeleka misaada yoyote kwa watu wa eneo.

Je, unatamani makampuni mbalimbali yangetoa msaada wa intaneti ya bure 😆 😆 watu kuweza kuwasiliana kama wakati ule Kagera ilivyokumbwa na majanga?

Vyanzo: The Verge, Mobile World Live

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com