Amazon Inaandaa App (Anytime) Ya Kutuma Na Kupokea Ujumbe/Meseji!

0
Sambaza

Amazon ni moja kati ya makampuni makubwa sana duniani na hata mmiliki wake yupo katika orodha ya matajiri wakuu duniani.

Amazon ni kampuni kubwa sana la mtandaoni linalohusisha mambo ya kununua na kuuza bidhaa katika mtandao. Baada ya kampuni kupata changamoto nyingi kwa wapinzani wake wakuu (ebay na alibaba) kampuni imelazimika kuleta maboresho ya kina ili kuhakikisha inabakiza wateja wake na kuongeza wapya.

amazon

Logo Ya Kampuni Ya Amazon

Kwa sasa ripoti zinasema kuwa kampuni hiyo ipo katika mchakato wa kuanzisha App yake ambayo itakuwa inawezesha kutuma na kupokea ujumbe (meseji)

SOMA PIA:  Tahadhari: Password meters si za kuaminika kwa asilimia zote

App hii itaangalia sana katika kutuma na kupokea meseji za kawaida, simu za video na sauti, ku’share picha, watumiaji watakuwa na uwezo wa kuweka ‘filter’ katika picha zao au video. Matumizi ya ‘Sticker’ na mfumo wa GIF utakuwepo na mambo mengine mengi.

Chanzo, AFTV News Kimesema Kuwa App Ya Anytime Itakuwa Na Mambo Yote Haya

App hii ikija hivi hivi ina uwezo mkubwa sana wa kushindana na zile ambazo zipo katika soko hivi sasa kama vile Facebook Messenger, WhatsApp na zingine.

SOMA PIA:  Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi

Kingine ni kwamba huduma hii itakuwa na ulinzi wa juu na usalama wa aina yake na hivyo itaweza kufanya kazi katika vifaa vya mikononi na hata katika kompyuta.

Amazon tayari imeshaweka mipango madhubuti ya kuliwezesha hili, kumbuka pia hapo awali walitangaza App ya Chime ambayo dhumuni lake ni kushindana na Skype kwani inatoa huduma za kupiga na kupokea simu za kawaida na za video. Dhumuni lake kubwa ni kuwezesha zile simu katika mikutano hasa katika ofisi.

SOMA PIA:  Taarifa za mitandao ya kijamii ya Wachina wanaoingia Marekani kuangaliwa

Ningependa kusikia kutoka kwako wewe Amazon unawapa maksi gani mpaka hapa kati ya mia? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Pia Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com