Drones za Amazon zinazotumika kusambaza vitu kwa wateja

0
Sambaza

Baada ya Amazon kufanikiwa kupata idhini kutoka kwa serikali sasa wanatuma drones kupeleka vitu mbalimbali mahali husika.

Mamlaka ya Anga nchini Uingereza imepa ruhusa kampuni maarufu ijulikanayo kama Amazon kutumia ya drones kama sehemu ya kupeleka bidhaa zilizoagizwa na wateja; badala ya mteja kwenda ofisi za Amazon kuchukua mzigo wake sasa mteja analetewa mzigo wake kwa kutumia ndege isiyo na rubani mpaka mahali alipo.

Amazon

Ndege isiyokuwa na rubani inayomilikiwa na Amazon.

Kitendo cha Amazon kukutumia drones ilikwa ni ndoto ya Bw. Jeff Bezos ambaye alikuwa akitaka sana kuona Amazon ikiwafikishia wateja bidhaa ndogondogo kwa kutumia drones ndani ya dakika 30.

Jinsi inavyofanya kazi

Ikishafika kwa mlengwa (anayeletewa mzigo) inatua kwenye kitambaa maalumu ambacho mteja anakuwa amekiandaa ili drone hiyo ikishafika iweze kutua kwenye kitambaa hicho kuweza kuzuia kutopata itilafu kutokana na kutua sehemu ambayi inaweza kuisababishia matatizo.

Drone kadhaa zilifanyiwa majaribio lakini drone ambayo inapendwa ni ile yenye uwezo wa kuwa ndege/helikopta pia yenye uwezo wa kwenda Km 80 kwa saa au kuruka umabli wa mita 100 kutoka ardhini.

Amazon frone wakati wa kutua

Amazon drone wakati wa kutua

Lengo ni kufanya drones hizo kutua katika hali ya ukimya sana na hazina kamera ila zina sensors. Malengo mengine ni kuhakikisha drones hizo zinafanya kazi katika mazingira salama ambayo yanatarajia kufikiwa ifikapo mwaka 2020.

Amazon drone ikipeleka mzigo kwa mteja.

Amazon drone ikipeleka mzigo kwa mteja.

Matatizo makubwa 3 ambayo drones hizo yanakumbana nayo.

Hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro. Amazon drones inakumbana na matatizo matatu yafuatayo:-

  • Drones hizo kwenda umbali ambao upeo wa macho hauwezi kuona. Kwa sheria za sasa zinamtaka muongozaji wa ndege kuweza kuona ndege anayoiongoza muda wote.
  • Kutengeneza drone ambazo haziwezi kugongana na kitu chochote; ni kama gari linalojiendesha lenyewe linalotegemea sensors ili lisiweze kugonga.
  • Kutengeneza drones nyingi kuongozwa na mtu mmoja; mtu mmoja anakuwa na mamlaka ya kuongoza drones nyingi.
SOMA PIA:  Samsung yafanya majaribio ya teknolojia ya 5G

Kila kitu kina changamoto zake, ni matumaini yetu sisi kama TeknoKona Amazon watatua matatizo hayo na kuboresha drones hizo. Tutaendelea kuwataarifu mengi kuhusu hili pale tutakapopata habari.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com