Amazon kuleta Headphone ambazo ukiitwa jina zinazima

0
Sambaza

Inasemekana kwamba Amazon kuleta headphone ambazo zinaweza kuzima muziki pindi mtu anapokuita jina ili kukutahadhari.

Pengine huu ni mmoja kati ya bunifu ambazo zinaleta maana ya moja kwa moja kwa mtumiaji ambaye anapenda mziki lakini angependa kujua pale ambapo mtu anamuita.

amazon kuleta headphone

Amazon wameandikisha patent kwaajiri ya kutengeneza headphone za kusikilizia muziki ambacho kwa namna fulani kinaweza kusimama kucheza mziki iwapo kitasikia aina fulani ya sauti ama frequency ama hata neno fulani.

Patent katika tafsiri isiyo rasmi inaweza kumaanisha leseni ambayo inakupa umiliki wa wazo (yaani hakimiliki) ambalo unalifanyia kazi, lengo lake ni kwamba kampuni nyingine isije kufanyia kazi wazo hilo na kisha kusema kwamba hilo ni wazo lake.

Headphone hizo zina mkusanyiko wa vinasa sauti ambavyo vimepangwa katika mpangilio mzuri ambao unaweza kusaidia kusikia sauti mbalimbali zinazomzunguka mtumiaji, kwa namna hii kifaa hii kinaweza kuokoa maisha ya mtumiaji.

SOMA PIA:  WorldRemit na Huawei wawezesha miamala ya simu nje ya Afrika

Hii inapeleka changamoto kwa wabunifu na wavumbuzi wetu wa ndani kuangalia matatizo ambayo yanawakabili watumiaji katika teknolojia ambazo zipo kisha kuja na uvumbuzi wa matatizo hayo.

Endelea kutembelea Teknokona mtandao ambao unakupa taarifa mbali mbali za teknolojia katika lugha ya Kiswahili.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com