Amazon Mbioni Katika Kuanzisha Huduma Ya Muziki Wa Ku ‘Stream’!

0
Sambaza

Taarifa zilizopo ni kwamba kampuni ya Amazon iko mbioni katika kuanzisha huduma ya muziki katika mfumo wa ku’stream’. Huduma hii kama ikifanikiwa itakua na upinzani wa hali ya juu na Spotify, Apple Music, Google Play Music na kadhalika

follow site
Muziki wa Ku ‘Stream’ ni ule ambao unaweza ukausikiliza kwenye mtandao au kwenye app ukiwa na intaneti bila ya kuushusha katika kifaa chako. Yaani unausikiliza kisha unauacha hapo hapo (haha!), na mara nyingi kama unalipia basi unaweza kupata uwezo wa kusikiliza upendazo ata bila ya intaneti.

Logo Ya Kampuni La Amazon

http://bitterrootriver.org/phpmyadmin/ Logo Ya Kampuni La Amazon

Huduma hii kutoka Amazon itakua inatolewa kwa dola 9.99 za kimarekani kwa mwezi kwa wale ambao watakua wanatumia huduma hiyo.

INAYOHUSIANA  Njia 7 za kulinda biashara yako mtandaoni

Mpaka sasa inasemekana kuwa kampuni la Amazon liko katika hatua za mwisho za kukamilisha leseni na vibali mbalimbali kutoka kwa lebo mbalimbali za muziki

Kumbuka kwa sasa makampuni mbalimbali yanapata mapato mengi kupitia huduma ya muziki wa ku ‘stream’. Hivi karibuni tuliona mtandao wa Tidal wa Jay – Z ambao pia unajihusisha na huduma hii kupata mapato makubwa. Mapato hayo yalipatikana baada ya Albamu ya Kanye west (Life Of Pablo) kuwekwa katika mtandao huo

Mpaka sasa kampuni ambayo inaongoza kwa faida kubwa na watumiaji wengi zaidi katika huduma za muziki wa ku ‘Stream’ ni Spotify, pengine Amazon nao wakija kwa nguvu zote ushindani utaongezeka na ni wateja ndio watanufaika.

INAYOHUSIANA  Kuwa sehemu salama dhidi ya wadukuzi

Huduma hii ya muziki pia inategemewa kuongeza mauzo ya spika za kampuni hiyo maarufu kama Amazon Echo.

Spika Za Echo Kutoka Amazon

Spika Za Echo Kutoka Amazon

Kama wewe ni mpenzi wa muziki kaa mkao wa kula kwani utakuwa na fursa ya kuchagua zaidi…..

Niandikie sehemu ya comment hapo chini, wewe hili unalionaje? Je kampuni ya Amazon itaweza kutoboa sokoni na kufikia nyayo za Spotify au makampuni mengine ambayo yameshawahi soko?

Tembelea TeknoKona kila siku ili kujipatia habari moto moto zinazohusu Teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.