AmpMe: App Inayogeuza Simu Janja Kadhaa kuwa Spika Zikipiga Wimbo Mmoja

0
Sambaza

Je unafikiria kuwa na kajisherehe /kaparty na marafiki au ndugu na hakuna spika za maana za kutumia?

Ifahamu app ya AmpMe yenye uwezo wa kugeuza simu kadhaa kutumika kama spika zote zikicheza mziki unaopigwa kutoka kwenye simu moja.

ampme-app

App hii inaweza pakuliwa kwenye simu janja au tableti, ikiwa inatumia Android au iOS.

Ili linawezekanaje?

Pakua app ya AmpMe katika simu na tableti zote unazotaka kutumia kama spika- hii ni pamoja na unazomiliki wewe na ata marafiki.

Chagua simu au tableti ambayo ndio ina nyimbo unazotaka zipiga,ingia kwenye app ya AmpMe na anza kupiga mziki kwa kubofya ‘START A PARTY’, chagua wimbo au album na kisha ‘play’.

Utaona chaguo la ‘Party Code’, wapatie wengine code hiyo na waiingize katika app ya AmpMe katika simu zao… basi muziki utaanza kusika mara moja kutoka kwenye simu zao.

AmpMe

Mara baada ya hilo kufanyika tayari muziki unaoucheza utaweza kusikia katika simu na tableti hizo zingine zote. Kumbuka huduma hii inatumia huduma ya intaneti, hivyo hakikisha na MB kadhaa kwenye simu au tableti zote zinazotumika.

SOMA PIA:  Snapchat Kuleta 'Link' Na 'Background' Katika Stories!

Unaweza ipakua app ya AmpMe kupitia soko la Google Play na AppStore bure kwa kubofya -> AmpMe | Google PlayStore / AmpMe | AppStore(iOS)

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com