Android Instant Apps: Tumia apps za Android bila hata kuzipakua (install)

0
Sambaza

Google wapo katika majaribio ya teknolojia yao kwa ajili ya watumiaji wa simu za Android itakayowawezesha watumiaji kutumia apps mbalimbali bila ata ya kuzipakua (install) kwenye simu zao.

android instant app

Teknolojia hiyo iliyopewa jina la Android Instant Apps kwa sasa ipo katika majaribio na apps maarufu kama vile BuzzFeed, Periscope, Viki na Wish zinahusishwa ila Google wamesema muda si mrefu wataongeza apps nyingi zaidi.

Teknolojia hii itaondoa ulazima wa watumiaji kupakua apps mbalimbali wasizozitumia mara kwa mara na hivyo kuwasaidia kuokoa nafasi (space) katika ujazo wa simu zao.

SOMA PIA:  Infinix na toleo la Infinix Note 4 Pro

Android Instant Apps ni nini hasa?

android instant apps

Jinsi Android Instant Apps inavyofanya kazi

  • Mfano utaweza kwenda Google Search na kutafuta app ya JamiiForums (ukiwa bado haujaipakua kwenye simu yako)
  • Kwa kubofya kwenye link(URL) yake app hiyo itafunguka mara moja kwa kutumia huduma ya intaneti bila ya uhitaji wa kupakua app nzima kwenye simu yako
  • Utaweza kufanya vyote vinavyoweza fanyika katika app hiyo na ukishaifunga tuu basi data zake zote zitafutika katika simu yako.
  • Hii itawezesha mtu kuweza kutumia apps nyingi bila uhitaji wa kuzipakua kwenye simu yako (pia unaweza ata ukajaribu app kabla ya kujiridhisha na kisha kuipakua kwenye simu yako)
SOMA PIA:  Skype yaingia mkataba na Paypal; sasa watumiaji wataweza kutuma pesa.

Kumbuka app hiyo ikifunguka katika mfumo wa Instant Apps basi itatumika data kidogo tuu (ukilinganisha na kama ungeipakua kabisa) na utaweza kufanya chochote ambacho kinaweza fanyika katika app hiyo kama vile imeshapakuliwa.

Unamtazamo gani juu ya teknolojia hii?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com