Tuma Mafaili Kati ya Android na Kompyuta Bila Waya Kirahisi

0
Sambaza

Kama wewe ni mtumiaji wa Android basi inawezekana tayari unajua kwa kiasi gani mfumo huu huru unavyobadilisha jinsi tunavyotumia simu zetu katika zama za sasa. Mara nyingi tuna- tuma mafaili kati ya android na kompyuta kwa kutumia waya.

Hii ni njia haraka zaidi kwa mafaili makubwa ila je, kuna njia rahisi zaidi ya kufanya hivyo, hasa ukiwa mbali na kompyuta? Tumepata mbili kwa ajili yako.

Utakachohitaji:
Es Explorer : Kwa ajili ya kutuma mafaili kwa mtandao wa eneo la karibu(LAN) na FTP.
ES Explorer Remote Manager: Kwa ajili ya kufanya simu yako kuwa ‘seva ya FTP’ na kuhamisha mafaili kwa njia ya FTP.

Es Explorer

Es Explorer ni app ya Android tulioielezea kama app muhimu ya kushughulikia mambo mengi kwenye simu za Android. Moja ya vitu hivyo ni ku- tuma mafaili kati ya simu na kompyuta. Es Explorer inasaidia kufanya hivi kwa njia za LAN na FTP.

SOMA PIA:  Apple yathibitisha kuwa inatengeneza magari.

Hamisha kwa LAN:

 • Kwanza, hakikisha kwamba kompyuta yako ina faili la ku-shirikishana (shared folder) ambalo unataka kutumia kwa ajili ya vitu kati yake na kifaa kingine au mtu mwingine. Unaeweza pia kubadili mipangilio ya kushirikisha ili uweze kutumia diski flani au kabati (folder) utakalo.
 • Pili, Hakikisha simu na kompyuta yako zimeungana na wayalesi iloyopo au ya kurusha kutoka kwenye simu yako.
 • Kwenye androidi yako, fungua ES Explorer na elekea kwenye menu ya kushoto na fungua kipengele cha Network->LAN.wpid-2015-03-18-13.49.58.png.png
 • Bonyeza ‘scan’ kupata orodha ya kompyuta zilizomo kwenye mtandao eneo la karibu au unaweza kuingiza anuani za kompyuta unayotaka kwa ‘ku-add server’ kwa kubonyeza ‘New’ kwenye menu ya chini.
 • Bofya kompyuta yako na weka jina na pasiwedi yako kama unavyotumia kuingia kwenye kompyuta yako. Ukifanikiwa, androidi yako itakuwa na uwezo wa kuona, kupakua na kuweka chochote kilicho kwenye diski au kabati iliyoshirikishwa na kompyuta hiyo.Screenshot_2015-03-18-18-13-56
 • Unaweza sasa kurudi kwenye kipengele cha ‘Local’ cha ES Explorer na kuhamisha mafaili unayotaka kwenda kwenye kompyuta.
SOMA PIA:  Hatimaye mwanzilishi wa Android azindua simu yake ya Essential

Hamisha kwa FTP:

Remote Manager

Remote Manager ni kipengele kidogo chenye uwezo wa kufanya simu yako ya mkononi ya Androidi kuwa seva ya FTP.

Kufanya simu kuwa seva

 • Ingia kwenye kipengele cha Remote Manager.wpid-2015-03-18-18.52.06.png.png
 • Kwenye menu ya chini bofya ‘Settings’ na weka mpangilio unaokupendeza zaidi, kisha rudi na bofya ‘Turn On’ kuanzisha seva yako. Utaona pia anuani ya seva hiyo.
 • Weka njia ya mkato ili kila uwashapo simu na kompyuta kwenye mtandao huu zijiunge moja kwa moja.
SOMA PIA:  Uzalishwaji wa maji yaliyopo hewani! #Sayansi #Teknolojia

Kuhamisha Mafaili kwenda kwenye Simu

  • Kwa urahisi, weka njia ya mkato ya simu yako kwenye kompyuta yaako ya Windows kwa kuingia My Computer, bonyeza kitufe cha Kulia kwenye kipanya kwa ajili ya menu alafu chagua ‘add a network location’ kama inavyoonesha picha hapa chini.

image

  • Ingiza anuani ya IP, jina na pasiwedi kama ulivyoziainisha kwenye Remote Manager na utakuwa na idhini ya kuona, kuchukua au kuweka mafaili unayotaka kwenye simu yako.

image

image

image

image

Tunatumaini tumekuongezea ujanja leo wa kuweza kufanya mawasiliano kati ya kompyuta na anroidi yako rahisi zaidi. Una maswali? Maoni? Usisite kuwasiliana nami kupitia eric@teknokona.com na pia kutpitia mitandao yetu ya jamii facebook, twitter na instagram.

 

Picha Na: HowToGeek , technologypress

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com