App 10 Bora Za Kupakua Katika Simu Ya Android – Agosti 2016!

0
Sambaza

Kuna zaidi ya App milioni 2 katika soko la Goolge Play kwa wale watumiaji wa Android. Baadhi ya watu huwa wanapata shida katika swala zima la kuchagua ni App zipi bora kuliko zingine.

Leo TeknoKona inakuletea App 10 bora za kuwa nazo katika kifaa chako cha Android. Sawa kuna zingine nyingi lakini kwa mtazamo wetu hizi ni kali zaidi

1. Pocket

App Ya Pocket -Hifadhi Sasa, Soma Baadae Hata Kama Hauna Huduma Ya Intaneti

App Ya Pocket -Hifadhi Sasa, Soma Baadae Hata Kama Hauna Huduma Ya Intaneti

Moja kati ya App za kuwa nazo ni Pocket, hilo halina ubishi (haaha)!. Pocket kazi yake kubwa ni kuwa kama mfuko wako ambao utaweka kila kitu ambacho unataka kukisoma/kukitazama baadae. Kwa mfano kama unakaribia ingia katika mkutano na ukaona makala katika mtandao wako wa TeknoKona unaweza hifadhi makala hiyo katika App ya Pocket alaf baadae ukaja kuipitia.

Kumbuka kila siku huwa unaingia katika mtandao ili kupata habari na taarifa zingine inaweza ikawa kifaa chako kikawa na chaji ndogo, App kama hii ndio inakuja kuwa msaada mkubwa kwako. Ukiachana na hili kuna faida nyingi sana za kuwa na App hii. Ili kuipata kwenye Simu ya Android ingia hapa

2. Prisma

Tumia App Ya Prisma Kutengeneza Picha Za Kijanja

Tumia App Ya Prisma Kutengeneza Picha Za Kijanja

Unaweza ukawa umeshaisikia hii App, Prisma. App hii inatumika katika kuhariri picha zako. Kwa haraka haraka inazifanya picha zako kazi ya sana, App hii inabadilisha kabisa muonekano wa picha yako na inaifanya ionekane kama imechorwa na mtaalamu (msanii).

Ni rahisi sana kuitumia cha kufanya hapa ni kupiga picha kwa kutumia App au tumia ile ambayo ulishaipiga na kisha chagua muonekano unaoutaka. Kuipata App Ya Prisma kwa mtumiaji wa Android ingia hapa.

SOMA PIA:  Google yaongeza lugha ya kiswahili katika voice search

3. App Kutoka Kampuni Ya Facebook

App Maarufu Kutoka Kampuni Ya Facebook

App Maarufu Kutoka Kampuni Ya Facebook

App kutoka kampuni la Facebook hazihitaji maelezo sana kwani nina uhakika kila mmoja wetu anatumia japokuwa moja ya App zao. Kumbuka kampuni ya Facebook wana App ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambazo ndio homa ya dunia kwa sasa. App hizo ndio zinazotikisa katika mitandao ya kijamii kwa sasa.

Ukitaka kushusha App hizo ingia hapa >>> Facebook, Instagram, WhatsApp. Lakini je hizo ndio homa ya jiji peke yake? Aaaaah nimekumbuka kuna na hii Snapchat japokuwa haimilikiwi na kampuni la Facebook.
4. skype

Skype - App Maarufu Kwa Simu Za Video Na Sauti

Skype – App Maarufu Kwa Simu Za Video Na Sauti

kwa wale ambao wanapenda App za kupiga simu za video, Skype bado ni App bora ya kuwa nayo. Skype ni moja kati ya huduma maarufu sana za kupiga simu za video duniani. Kutokana na skype huduma nyingi sana zilianzishwa na kuboreshwa. Unataka kumuona unaempigia – hakikisha na yeye ana skype — simu? Shusha Skype hapa

5. google translate

Google Translate -Tafsiri Zaidi Ya Lugha 29 Kwa Kutumia App Hii

Google Translate -Tafsiri Zaidi Ya Lugha 29 Kwa Kutumia App Hii

kuwa na mkalimani wako karibu, kumbuka Gooogle Translate inatafsiri lugha zaidi ya 29. Ukiwa na App hii unaweza ukatafsiri lugha kadhaa tena kwa kutumia kamera ya simu janja yako. Cha kufanya ukiona kuna neno la kigeni limeandikwa sehemu chukua simu, fungua App na kisha lengesha kamera katika eneo hilo na Google translate itatafsiri kuja katika lugha unayoitaka. Unataka kuwa karibu na mkalimani wako? Pakua Google Translate hapa

SOMA PIA:  Teleprompta: Teknolojia ya kusoma habari katika televisheni na hotuba za viongozi

6. Google Drive & Drop Box (Hifadhi Mafaili Katika Mtandao)

Hifadhi Mafaili Yako Mtandaoni Kwa Kutumia App Za DropBox Na Google Drive

Hifadhi Mafaili Yako Mtandaoni Kwa Kutumia App Za DropBox Na Google Drive

App muhimu sana za kuwa nazo katika vifaa vyako (simu au hata kompyuta) ni hizi. Google Drive au Drop box kazi zake ni moja tuu, zitakuwezesha wewe kuhifadhi mafaili yako katika mtandao na kuyachukua muda wowote unapoyahitaji ili mradi tuu uwe na huduma ya intaneti.

Hebu fikiria kama simu yako imeibwa na ulikuwa umehifadhi vitu kama vile picha na nyimbo katika huduma hizi? Inamaanisha kuwa mfaili hayo unaweza ukayapata tena. Shusha Google Drive Hapa na Dropbox hapa.

7. Currency XE

Currecy XE - App Inayokujulisha VIwango Vya Kigeni

Currecy XE – App Inayokujulisha VIwango Vya Kigeni

Ukiwa na App hii utaweza kulinganisha fedha za kigeni na za nchi yako au nchi nyingine ili kujua ni shilingi ngapi kwa wakati huo. Hivi ni maran ngapi umeuliza au rafiki yako amekuuliza kuwa dola moja ni shilingi ngapi ya Tanzania? Ukiwa na App kama hii maswali kama hayo huwezi ukauliza. App hii ni ya muhimu hata kwa wale ambao wanasafiri nje ya nchi Ili kuipakuwa ingia hapa

8. Android Device Manager

kama ikitokea umepoteza au kifaa chako cha Android kimeibwa ukiwa na App ya Android Device Manager unaweza ukakipata. kinachofanyika hapa App hii itakusaidia kujua eneo la kifaa chako kilipo.

Licha ya kuwa unaweza ukajua mahali kilipo bali pia unaweza ukakiloki kifaa hicho kwa kutumia taarifa za akaunti yako ya Google, pia unaweza ukafuta taarifa za kifaa chicho (mfano unaweza ukafuta taarifa zote katika simu). Hata kama una kifaa zaidi ya kimoja App hii itakuwezesha kujua vyote viko wapi kwa wakati huo.

SOMA PIA:  Simu za Samsung Galaxy kuanza kupata toleo la Android Oreo 2018

Hii ni moja ya vitu muhimu sana kuwa navyo katika simu yako. Ili kuipakua katika kifaa chako inigia hapa

Android Device Manager simu ya android

Android Device Manager

9. Google 

Moja kati ya App maradufu kabisa za kuwa nazo katika simu janja yako yako ya Android ni Google. Ingawa wengi wataona ni sawa tuu kuingia katika mtandao wa Google kwa kutumia kivinjari (bila kutumia App hii) lakini bado kuwa nayo katika simu janja yako ni vizuri zaidi.

Google  itakurahisishia kufanya kazi mbalimbali ambazo huwa unazifanya katika mtandao wa Google kwa haraka zaidi. Hapa utapata taarifa mbali mbali (habari, michezo n.k) kwa haraka zaidi. Pia kama kawaida utaweza kuiuliza Google maswali mbalimbali (haahaha)!. Ili kuipakua katika simu janja yako ya Android inabidi  kuingia hapa

Google

Google

10. Hakiki

Nimeshangazwa na matumizi ya App hii na kilichonivutia zaidi ni kwamba katengeneza Mtanzania Mwenzetu. Ni jambo la kujivunia sana, App hii inakuwezesha kufahamu taarifa za matumiza ya pesa zako katika mfumo wa simu (Mobile Money).

Taarifa zako zote za M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na zingine nyingi zinazohusisha pesa katika simu yako kwa mfano ununuzi wa umeme, vocha kwa kupitia njia ya ‘Mobile Money’ utaziona katika App hii. App  imetengenezwa na kampuni inayojulikana kama Nabure. Ukitaka kufahamu zaidi kuhusiana na App hii soma hapa. Umeshaisoma sio, sasa unaweza ukaishusha hapa

Hakiki App

Hakiki

hakika app

Muonekano wa ripoti katika makundi ya huduma mbalimbali

Kwa leo tumekuleta hizi, Kama kuna nyingine ni nzuri na unahisi inaweza kuwa katika listi hii niandikie hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako.

Tembelea mtandao wako pendwa wa  TeknoKona kila siku ili kujipatia habari na maujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona Diama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com