App 5 Za Kuingia Nazo Mwaka 2016 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

App 5 Za Kuingia Nazo Mwaka 2016

0
Sambaza

Mwisho wa mwaka umewadia. Tunaposherekea na kumshukuru Mwenyeenzi Mungu, ni vyema kufikiria ni jinsi gani tutapiga hatua na kuwa vizuri zaidi ya mwaka huu. Makala hii ya kufunga mwaka imeandikwa kuwapa dira, japo kidogo watu wetu mnaofuatilia teknolojia kimakini, na hasa apps, ili tuwasaidie na kufikisha malengo yenu kuelekea Mwaka mpya wa 2016.

Offtime

image

Simu za mikononi zimeleta taarifa na habari karibu zaidi kuliko kipindi chochote cha maisha ya binadamu. Wakati mwingine ni vigumu kuiacha simu na kufanya mambo mengine. App ya Kujizuia kutumia simu utakavyo ni muhimu sasa, iwapo unataka kuanza mwaka ukiwa unafanya mambo mengi zaidi na kuyafanikisha. App kama hizi zinaitwa, “e-detoxicating apps”. Offtime ni app rahisi kutumia iwapo ungependa ujibane zaidi ili ufanye mambo mengi zaidi ya kujijenga.

INAYOHUSIANA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Pocket

pocket-emailPocket ni app inayokuwezesha kuhifadhi unachokiona mtandaoni ili uweze kusoma baadae. Kwa kutumia app kama Pocket, unaweza kupanga vizuri makala zako katika makundi unayopenda. Ukijikuta hutaki kuinamia skrini ya simu, unaweza kuifanya Pocket ikusomee makala zako kwa sauti. Pocket siyo tu app nzuri kuwa nayo, bali ni muhimu.

Google Keep

image

Pengine ndani ya mwaka mpya unataka usisahau mambo ya kibunifu unayoyawaza. Tumia app kama Google Keep kuhakikisha ubunifu wako upo nawe popote na haupotei kamwe.

mPaper

image

App inayotengenezwa kinyumbani imeweka historia mwaka huu baada ya kushinda tuzo za teknolojia nje ya nchi. Umepita wakati sasa wa kukosa sababu ya kununua gazeti. App ya M-paper imefanya mambo kuwa marahisi mno kwa mpenda magazeti. Faida ni nyingi unaponunua gazeti kupitia m-paper. Zaidi ya yote, utaokoa muda na pesa ya kupata magazeti.

INAYOHUSIANA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

http://impactse.com/temp1-1.php Heri ya mwaka mpya, 2016! Tunatumaini tutaendelea kuwa zaidi na wewe katika kona ya teknolojia Tanzania na Afrika Mashariki.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply