Unapigiwa simu za usumbufu na matangazo? Google na App ya kuzuia

Unapigiwa simu za usumbufu na matangazo? Google waja na App ya kuzuia

0
Sambaza

Google waleta na app itakayowasaidia watumiaji wa simu zake kuweza kuepukana na upigiwaji wa simu za usumbufu na matangazo kutoka huduma au watu wanaotaka kuwauzia bidhaa/huduma mbalimbali.

simu za usumbufu

Kuna muda unaweza ukaacha kufanya jambo la maana ukasogea pembeni kupokea simu unayodhani ni muhimu sana – kumbe ni matangazo tuu

Simu hizo maarafu kwa jina la kimombo la ‘spam calls’, ni tatizo kubwa sana katika nchi zilizoendelea kuliko ata kwa nchi zinazoendelea. Google wanatengeneza toleo spesheli la app ya kupiga na kupokea simu kwa matoleo ya simu ya Android One, Nexus na Pixel.

http://lifeincostamesa.com/costa-mesa-real-estate-agents-cut-fsbo-dilemmas/?share=email Android One, ni mradi spesheli wa Google unaohusisha utengenezaji wa toleo jepesi la programu endeshaji ya Android na kuyapatia makampuni ya utengenezaji simu yenye nia ya kutengeneza simu za bei nafuu bila kuathiri utendaji kazi wa simu.

purchase provigil from canada Nexus, ni familia ya simu za Android zinazobuniwa na kutengenezwa kwa ushirikano kati ya Google na makampuni mengine ya utengenezaji simu kama vile LG, Huawei, na wengine.

buy Keppra canada Pixel, ni familia mpya ya simu zinazotengenezwa na Google. Google wenyewe wameamua kuchukua nafasi kubwa katika ubunifu na kisha kusimamia utengenezaji wa simu za kiwango cha juu cha ubora zinazotumia Android.

simu za usumbufu

App hii pamoja na kazi hii pia inatumika kama app ya kupokea na kupiga simu, na kutumia orodha ya namba za simu/contacts

Je, uwezo huu utafanyaje kazi?

  • Namba ya simu ambayo imesharipotiwa na wengine wengi kama ni ya kutoka kwa huduma au mtu anayepiga simu za usumbufu akipiga simu;
  • App ya kupiga na kupokea simu, ‘Phone’, itaigundua na moja kwa moja kuilazimisha iache ujumbe wa sauti – voicemail.
  • Wewe kama mtumiaji simu hautapata notification/ujumbe wa kukuambia ya kwamba kuna simu imepigwa kwa wakati huo. Simu itakuwa kimya kama vile hakuna kilichotokea.
  • Ila ukiingia kwenye app yako ya kupiga na kupokea simu ndio utaona ujio wa ‘missed call’ kutoka simu hiyo, pamoja na kukuonesha kama ujumbe wa sauti/voicemail uliachwa.
INAYOHUSIANA  Samsung kuwekeza zaidi kuimarisha bidhaa zake

Google wanategemewa kutumia teknolojia ya akili-feki-ya-kompyuta (AI), kuweza kutambua namba za simu mbalimbali zinazochukuliwa kama SPAM. Tayari teknolojia yao katika kuchambua barua pepe hasa hasa kupitia huduma yao ya barua pepe ya Gmail inauwezo mkubwa wa kuzidi kusaidia kufanikisha kazi ya app hii.

Kwa sasa uwezo huo upo katika majaribio, ya kiwango cha BETA. Wengi wanategemea uwezo huo mpya utaanza kusambaa kwa watumiaji wengine wa simu za Android One, Nexus na Pixel.

Kama unatumia moja ya simu zenye sifa hii basi unaweza tembelea Google PlayStore hapa – Google PlayStore -> Download Google Phone

Usiogope kama hautimii simu hizo, tunaamini muda si mrefu Google kupitia toleo la Android wanaweza kuleta huduma hii kwa watumiaji wengi zaidi.

INAYOHUSIANA  Google ina kifaa chake cha kudhibiti udukuzi

Je, ni simu za aina gani huwa haupendi kuzipokea ukipigiwa?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.