App ya Azam TV yaanza kupatikana rasmi

0
Sambaza

App ya Azam TV. App ya kisasa kabisa ya AzamTV imeanza kupatikana rasmi katika Google Play Store na App Store ya Apple kuanzia Julai Mosi.

App hiyo iliyokuwa ipatikane tangu Juni mosi lakini ilishindikana, watu wataweza kutazama chaneli saba ambazo ni Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu, ZBC 2, Azam Sports HD kwa Tanzania Pekee, na Real Madrid TV na NTV Uganda.

App ya Azam TV

App ya Azam TV

Taarifa moto moto za Kimichezo, Habari, Burudani na matukio mbalimbali yanayoendelea nchini na ulimwenguni pia yatapatikana kupitia App hiyo.

SOMA PIA:  Facebook Messenger: Jinsi ya kutafuta ujumbe uliotoweka

Kwa sasa Kuangalia chaneli hizo hakutatozwa pesa yoyote yaani ni bure ingawa mwanzoni ilitaarifiwa kulipia kwa Tsh 400 kwa siku, Tsh 2500 kwa wiki au Tsh 9000 kwa mwezi.

App ya Azam TV

App ya Azam TV

Ili kuweza kufurahia huduma zao, hakikisha una bundle la kutosha tu na network nzuri ili uweze kufaidi vizuri huduma zao mahali ulipo na wakati wowote.

3G ndio mtandao wa chini kabisa unaotakiwa kuutumia kupata huduma hii kwenye AzamTV app.

SOMA PIA:  Kivinjari cha UC Browser charudishwa soko la Apps la Google Play Store

Kituo kingine cha Runinga ambacho kilishatangaza App yao ni ITV ambayo inapatikana Google Play Store na App Store ya Apple

Link ya AzamTv katika Play Store

Link ya AzamTv katika App Store

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com