Kampuni yashtakiwa kutokana na Headphones zinazofanya ujasusi kwa watumiaji wake

0
Sambaza

Katika hali ya kawaida unaweza ukawa hutaki kila uchokisikiliza wengine wakisikie au usiwakwaze wale walio karibu na wewe kwa kile unachokisiliza hivyo unaamua kutumia headphones.

Usalama na usiri wa taarifa zako ni moja ya vitu ambavyo kila mtu anatakiwa kuheshimu kwa namna yoyote ile kutokana na kwamba mhusika ndiye anayejua uzito na umuhimu wa taarifa zake na kwamba mtu mwingine hafai kujua.

Kampuni moja imejikuta matatani baada ya mmoja ya watu walionunua headphones za kampuni hiyo kubaini kuwa headphones hizo kwa kupitia app yake inasambaza taarifa za mhusika kwenye tovuti mbalimbali.

Bose headphones ambayo ili kupata ladha nzuri ya kile unachokisiliza unatakiwa kupakuwa app yake kutoka Play Store/App Store na baada ya kuifungua app hiyo itakuomba ujaze taarifa kama barua pepe, jina lako na namba za kipekee (serial number) za headphones zako.

Soma pia: Apple yanunua Beats by Dre

SOMA PIA:  Kampuni ya Sadolin Tanzania imenunuliwa, sasa kufahamika kama Plascon Tanzania

Ubaya wa app hii ni kwamba inachunguza taarifa binafsi na kusambaza kwenye mitandao kama Segment.io ambayo inatumia tovuti yake inakusanya taarifa mbalimbali na kuzituma popote pale.

 Headphones zinazofanya ujasusi

Kampuni yashtakiwa kutokana na Headphones zinazofanya ujasusi kwa watumiaji wake: Headphones zisizotumia waya zinazomilikiwa na Bose Corp.

Mmoja ya watu walionunua headphones hizo ameifungulia mashtaka kampuni yo na kutaka haki ipatikane. Kampuni hiyo inakadiriwa kupata faida ya $3.5 bilioni kwa mwaka kutokana na mauzo ya QuietComfort 35, QuietControl 30, SoundLink Around-Ear Wireless Headphones II, SoundLink Color II, SoundSport Wireless na SoundSport Pulse Wireless.

Taarifa zako hazipaswi mtu mwingine kuzijua bila idhini ya mhusika kwahiyo ni vyema kusimama imara na kutetea haki yako. Tuambie, wewe unamiliki headphones za Bose? Ulikuwa unajua kuwa taarifa zako hazipo salama?

Vyanzo: Reuters, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com