App ya mPaper kutoka Tanzania Yashinda Tuzo Nchini Afrika Kusini

1
Sambaza

Tulishaandika kuhusu app maarufu ya kununua, kuhifadhi na kusoma magazeti kupitia simu au tableti yako ifahamikayo kwa jina la mPaper kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za ubunifu wa Apps za Afrika.

App hiyo imenyakua tuzo ya app bora ya Kiafrika (Best African app), ilikuwa inashindana na app nyingine nne kutoka nchini Afrika Kusini, Senegali, na Nigeria.

Bwana Edwin wa SmartCodes na mPaper akipokea tuzo hiyo

Bwana Edwin wa SmartCodes na mPaper akipokea tuzo hiyo

App hiyo iliyotengenezwa na inaendeshwa na kampuni ya mambo ya kidigitali ya SmartCodes imefanya suala la ununuaji, uhifadhi na usomaji wa magazeti na majarida mengine kuwa mrahisi mno. Watu wengi siku hizi wanatumia simu na tableti zao kama sehemu kubwa ya wao kusomea vitabu na habari mbalimbali na hivyo mPaper imerahisisha magazeti kuwafikia watu kwa njia rahisi na inayoanza kupendelewa zaidi na hasa vijana.

SOMA PIA:  Airtel, Tigo na Zantel warahisisha kutuma na kupokea pesa kwenye mitandao yao

App hiyo imenyakua tuzo ya app bora ya Kiafrika (Best African app), ilikuwa inashindana na app nyingine nne kutoka nchini Afrika Kusini, Senegali, na Nigeria. Tuzo zinazotolewa na TheAppsAfrica.com kwa mwaka huu ziliusisha maombi kutoka apps zaidi ya 200 kutoka nchi 21.

airtel tanzania bando

Muonekano wa app ya M Paper

Muonekano wa app ya M Paper

Kipengele kingine ambacho app hiyo ilikuwa inashindania ni pamoja na app bora katika ‘Eneo la Elimu’ – ‘Best Educational Innovation), hadi makala hii inaenda mtandaoni bado hatujapata kujua habari ya eneo hili, njoo baadae…kujua zaidi.

SOMA PIA:  Google Assistant sasa inaweza kujua jina la wimbo unaoimba kwenye simu janja #Masasisho

Timu ya TeknoKona inaipongeza timu nzima ya mPaper na kampuni ya SmartCodes, ni matengemeo yetu app hiyo isambae barani Afrika. Iongeze magazeti kutoka nchi nyingi zaidi na kuwawezesha waafrika kuweza kusoma gazeti la siku hiyo hiyo kutoka nchi jirani.

M- Paper | Google Play

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: App ya mPaper kutoka Tanzania Yashinda Tuzo Nchini Afrika Kusini | Teknolojia

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com