Youtube ni moja kati ya tovuti/app inayotembelewa kwa wingi sana sehemu nyingi duniani kuweza kuangalia picha jongefu (kwa Kiswahili sanifu) au video za vitu/mambo mbalimbali yaliyotokea na yanayotokea ulimwenguni.
Ni wazi kwamba watu wengi wanatembelea Youtube kwa kupitia simu janja kutokana na kwamba ndio kifaa (simu janja) ambacho kinakuwa karibu na kufungua Youtube kwa urahisi zaidi kuliko hata kwa kutumia kompyuta.
Jambo la kuangalia video kupitia kwenye simu janja halafu video inakuwa haienei kioo kizima (kwa simu janja zenye uwiano wa 16:8) hilo sasa limeboreshwa kwenye simu janja zinazotumia Android na zenye kioo cha uwiano wa 18:9.
Kwa simu janja kama Samsung Galaxy S8+ na LG V30 ni moja ya simu janja zitakazonufaika na maboresho haya kwenye app ya Youtube. Kwenye maboresho ambayo Youtube imeyafanya kwenye app yake upande wa Android hapo awali yalikuwepo tu kwenye simu janja za Google Pixel 2 XL.
Kilichoboreshwa ni kuweza kukuza picha mnato na kuenea kioo kizima hasa chenye uwiano wa 18:9. Lakini Youtube inafanya mpango hata wenye simu janja chini ya uwiano wa 18:9 kuweza kukuza video na kuenea kioo kizima cha simu zao.
Ni toleo la Youtube v12.43 ndio lenye maboresho hayo ya kwenye app ya Youtube upande wa Android na kama simu janja yako haina toleo hilo ni vyema ukafanyia masasisho app ya hiyo au ukapakua programu ndogo ya Youtube iliyo katika mfumo wa>>>APK kuweza kupata toleo la Youtube v12.43.
Vyanzo: 9To5Google, Android Police, Gadgets 360