Apple Energy: Apple Kujikita Katika Teknolojia Ya Nishati!

0
Sambaza

Wengi tumezoea kuiona kampuni ya Apple ikiwa inajikita zaidi katika teknolojia ya simu na kompyuta, na kidogo suala la magari janja siku hizi…sasa imejiingiza katika sekta ya nishati.

Kampuni hiyo imetengeneza kiwanda kingine kinachojitegemea ambacho kitaweza kuzalisha umeme mwingi wa jua. Umeme huo utaisaidia kampuni katika ofisi zake na pia umeme unaobakia (unaozidi) wataweza wauzia watu wengine.

Kampuni mpaka sasa ina mashamba makubwa kabisa ya kufua umeme wa jua. Jina kamili la kampuni hiyo ya nishati ni Apple Energy LLC na inamilikiwa kwa 100% na Apple Inc.

SOMA PIA:  Simu ya LG G6: LG waonesha bado wapo makini na biashara ya simu

258E7F8900000578-2948238-image-a-6_1423625681689
Sio kitu cha achabu kuona kampuni ya Apple leo inakuja na nishati ya aina hii kwani tangia mwaka 2013 katika vituo vyake vyote vya data (data center) vilikua vinatumia umeme wa kufuliwa. Na mfano mzuri ni kwamba kampuni ina project yake yenye sola paneli zaidi ya maeneo 800 ambayo yanaendesha shughuli za kampuni huko Singapore.

Ukiachana na kutumia umeme waonaozalisha kupitia sola paneli zao, bado kampuni ina mpango wa kuyauzia makampuni mengine umeme unaosalia. Taarifa iliyopo ni kwamba kampuni itauza nishati hiyo kwa bei iliyopo sokoni muda huo.

SOMA PIA:  BarraCuda Pro: Diski uhifadhi ya ukubwa wa TB 12 kwa ajili ya kompyuta za mezani

Kampuni hiyo imeseama kuwa iko tayari na ina vigezo tosha vya kuuza umeme unaosalia kwa bei ile ile iliyopangwa sokoni kwa kuwa kampuni kama kampuni bado ni ngeni katika swala zima la kuuza umeme hivyo haitakuwa na nguvu ya kushawishi kupanda au kushuka kwa bei ya umeme katika soko.

apple energy

Paneli Ambazo Zinatumika Kufua Umeme Wa Jua

Kama inavyofahamika kuwa awamu hii mauzo ya simu za Apple maarufu kama iPhone yemeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na vipindi vyote vya mauzo ya matoleo ya simu za aina nyingine. Pengine labda hii ni njia nyingine kwa kampuni kuweza kupapasa kona zingine ili kujihakikishia uhakika wa mapato.

SOMA PIA:  IFA 2017 kufanyika kuanzia Septemba 1-6 jijini Berlin

Na pia kumbuka ni jambo zuri kutawanya biashara zako na kuwa na njia nyingi za kuweza kujipatia kipato.

Niandikie maoni yako au lolote ulilonalo moyoni hapo chini sehemu ya comment je swala hili wewe unalionaje? Je unaipongeza Apple au unahisi kuwa inaenda katika soko ambalo halijalikamata kama lile la simu?

Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari moto moto za kiteknolojia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com