Apple, Facebook na Google kuandika barua ya pamoja kwenda kwa Rais Trump - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple, Facebook na Google kuandika barua ya pamoja kwenda kwa Rais Trump

0
Sambaza

Makampuni nguli katika masuala ya teknolojia yameamua kuvunja ukimya hivyo wapo katika mchakato ya kuandika barua ya pamoja kwenda kwa Rais mpya wa Marekani.

click here

Finpecia 1 mg order online Uamuzi huo unafutia baada ya Rais Trump mnamo Jan 27 kusaini amri kuzuia watu kutoka click here mataifa 7 ya Kiislamu kwa kile alichokidai ni kwa sababu za kiusalama. Katazo hilo limeonekana kuwa mwiba kwa wengi kiasi cha kusababisha maandamano katika nchi mbalimbali.

Katika barua hiyo japo kwa uchache wamesema wanaunga mkono jitihada zake pamoja na serikali yake ila cha muhimu ni uwezo wa wafanyakazi wa Google, Apple na Facebook wanaotoka katika mataifa 7 ambayo yamewekewa vikwazo.

Mafanikio ya makampuni haya yenye ushindani mkubwa katika biashara hayapatikani kutokana na wafanyakazi wazawa tu bali mafanikio hayo pia yanatokana na wafanyakazi kutoka nje ya Marekani.

Apple , Facebook,  Google, Twitter, Microsoft na Yahoo  ndio makampuni yanayotarajiwa kutia saini katika barua hiyo.

Katika barua hiyo ambayo bado ipo Katika matayarisho haijaweka wazi mengi kwa umma ila kikubwa ni kwa makampuni hayo kupendekeza wafanyakazi wake kuweza kuingia/kutoka Marekani bila kizuizi chochote katika utekelezaji wa majukumu yao.

INAYOHUSIANA  Mkebe wa kuhifadhi AirPods kuwa na uwezo wa kuchaji iPhone

Barua hiyo ambayo itakuwa imebeba muhktasabali wa wafanyakazi ambao si wazawa wa Marekani itawasalishwa kwa Rais Trump mara baada ya kukamilika.

Je, Rais Trump atakubaliana na mapendekezo ya pamoja kutoka Facebook, Google na Apple?

Vyanzo: Fortune, mitandao mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.