Apple Imeachia iOS 8.3: Jicho Letu Katika Maboresho Yake! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple Imeachia iOS 8.3: Jicho Letu Katika Maboresho Yake!

0
Sambaza

ios 8.3

Apple imeachia iOs 8.3 ambayo ina marekebisho kibao ambayo yalikuwepo katika iOS 8.  iOS 8.3 kwanza ilikua iliachiwa katika Programu ya Apple Inayoitwa iOs Beta, na

baadae wakakubali kuachia ios hiyo kwa watumiaji wote.

Yafuatayo Ni Mambo Matano (5) Ambayo Apple Wamebadilisha Toka iOs 8 Mpaka 8.3

http://amidwifeonthepath.com/tools-of-my-trade-10/ 1. Emoja Mbalimbali Mpya Na Nzuri Zaidi

Kitu kikubwa kabisa katika mabadiliko yaliyofanyika katika iOs hii (8.3) ni mabadiliko juu ya Emoji katika keyboard za bidhaa za Apple. Keyboard hizo zinajumuisha zaidi ya karakta 300  na rangi mbali mbali za emoji zilizoongezeka na ambazo mtumiaji wa Apple anaweza badilisha yaani anaweza weka rangi ya ngozi yeye aipendayo. Katika Keyboard iliyopita Emoji zilikua zimejikita zaidi kwa mtu wa India kama unakumbuka vizuri kuna emoji ya mwanaume alikua amevaa kofia ya kihindi (turban), na watu wengine (Ukabila) hawakuwa wamewakilishwa. Apple pia wamefanya mabadiliko mengi juu ya mahusiano ya Emoji mfano emoji ya mashoga na wasagaji

INAYOHUSIANA  Miaka kumi ya App Store kwenye biashara

http://bitcoinsgreece.com/?wordfence_lh=1 SOMA ZAIDI: Apple Waleta iOS 8.3 Iliyojaa Emoji Mpya 

http://beautificationsociety.com/?p=107 2. iCloud Photos Library

Kutokana na kwamba kipengele cha ‘Photos’ kuwekwa katika OS X kuna njia moya mbali mbali juu ya jinsi picha zinavyoweza kuwa zinashughulikiwa katika iCloud. kitu hicho hicho kinaweza kuwa kinafanyika katika iOS ambacho kinahusisha kuhariri picha na kadhalika. Kipengele hiki hata hivyo iunabidi kiwashwe ki analojia ambavyo inawezekana kwa kwenda kwenye menu ya “Photos and Camera” katika Setting.

3. Muelekeo (Kugeuka Geuka) Wa Skrini Kuboresha

Tangia Apple waachie iPhone 6 na 6 plus, ilikua na dosari nyingi juu ya kugeuza skrini kuwa katika mfumo wa muonekano wa kulala (Landscape). kwa mfano watumiaji walikua wanapata tabu kugeuza skrini katika muonekano wa kawaida (portrait)  baada ya kuitumia katika mfumo wa mlalo (Landscape).Na piaa saa zingine wakati Skrini ikijigeuza huwa inakua chini juu. Lakini haya yote yatakuwa yamerekebishwa katika iOs mpya ya 8.3.

INAYOHUSIANA  Kicharazio cha kwenye MacBook na MacBook Pro kubadilishwa bila malipo

4. Maboresho Katika Connectivity (Maunganisho)

Kulikua na dosari ya maunganisho katika iOs ya 8.2. Kwa mfano watumiaji walikua wakiulizwa mara kwa mara kurudia taarifa zao za kuingia katika WiFi hizo na pia mara nyingi walikua wanasumbuliwa na kitendo cha kuwa ‘Disconnected’ katika WiFi hizo.

5. Maboresho Juu Ya CarPlay

CarPlay

CarPlay

CarPlay bado sio kitu maarufu sana lakini inakuwa kwa kiasi kikubwa sana na makampuni mengi ya magari yameamua kuweka kuweka kipengele hichi katika magari yao katika kipindi cha mwaka ujao. iOs 8.3 inawezesha iPhone kuwa tayari kwa magari haya.  Hii itawawezesha watumiaji wa magiri haya kutumia simu zao (iPhone) ku ‘connect’  katika CarPlay bila ya waya. Hapo mwanzo watumiaji waliweza fanya hivyo kwa kuunganisha nyaya kwenye simu mpaka kwenye gari. Sasa hii linawezekana wakati simu ya mtumiaji ikiwa mfukoni tuu.

INAYOHUSIANA  Apple na Oprah kufanya kazi kwa pamoja

Kujua Zaidi Kuhusu CarPlay Angalia Video Ifuatayo

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply