iPhone calibration - Apple kuruhusu rasmi makampuni mengine kurekebisha iPhone

Apple kuruhusu rasmi makampuni mengine kurekebisha simu zao

0
Sambaza

Imekuwa desturi ya kampuni nguli na inayofanya vizuri katika biashara ya vifaa vya kieletroniki kuwa wao tu wenye idhini ya kurekebisha simu (iPhone) kutoka kwenye kampuni yao pale ambapo mteja ataileta ili ifanyiwe matengenezo ya kitu fulani lakini hilo sasa lipo mbioni kubadilika  😯  😯 .

Vifaa vya kieletroniki kupata hitilafu si jambo la kushangaza na hivyo basi kuhitaji matengenezo aidha makubwa au madogo kulingana na ukubwa/udogo wa tatizo lenyewe. Hapo awali iwapo simu yako (iPhone) ikipata tatizo na ukaenda kwa fundi kwa ajili ya matengenezo basi ilimbidi fundi huyo achukue simu yako na kuipeleka katika duka la Apple ifanyiwe matengenezo halafu ndio akurudishie.

Simu ya iPhone ikiwa imechomekwa kwenye kifaa hicho

source site Apple sasa imeamua kuacha kuwa yeye tu kuwa na uwezo wa kurekebisha simu zake. Mashine zao spesheli (iPhone calibration machine) zinazotumika katika kufanikisha iPhone 6s na matoleo yaliyofuata baada ya iPhone 6s zimetolewa kwa kampuni 3 zilizoidhinishwa kuwa na uwezo wa kufanya matengenezo kwa simu kutoka Apple.

INAYOHUSIANA  Motorola inatarajiwa kutoa simu janja

watch Soma pia: Teknolojia ya 5G kutoka Apple

Uwezo wa mashine inayotumika kufanya matengenezo ya iPhone

iPhone calibration – baada ya simu kufanyiwa marekebisho ina uwezo wa kuhakiki mguso wa 3D pamoja na multi-touch ndani ya dakika  watch kumi na tano jambo linakubaliana na viwango vya Apple.

ComputerCare ni moja ya kampuni zilzopewa kibali na Apple kuzifanyia matengenezo iPhone. Kampuni nyingine mbili bado hazijawekwa wazi.

Kitendo cha Apple kurushu kampuni nyingine (Third party) ni jambo jema litakalopunguza kama si kuondoa kabisa ile adha ya kwenda kwenye duka la Apple ili simu yako iweze kurekebishwa na ni matumaini ya wengi kuwa vibali vitatolewa kwa wingi duniani kote.

Chanzo: Engadget, Softpedia

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.