Apple Kuachana na Matoleo ya iPhone ya GB 16! #Ripoti

0
Sambaza

Kuna ripoti zimezagaa mtandaoni zinazoonesha kuna uwezekano mkubwa wa toleo lijalo iPhone la chini kuwa na diski ujazo wa GB 32 badala ya GB 16 kama ilivyozoeleka kwa muda mrefu. Toleo la iPhone linalosuburiwa kwa sasa ni iPhone 7.

simu ya iphone  6s iPhone ya GB 16

Simu ya iPhone 6S

Kwa mara ya kwanza kabisa Apple kuanza kuja na matoleo ya iPhone ya GB 16 ilikuwa mwaka 2010 na ujio wa iPhone 4. Kuanzia hapo ndio kukawa na utamaduni wa kuwa na toleo la GB 16, na ni hakika ni mengi yamebadilika tokea mwaka huo. Apps zimekuwa nyingi sana….na pia zimekuwa za ‘size’ kubwa sana – kuna apps za hadi zaidi ya GB 1 kwa app moja.

SOMA PIA:  Nova Launcher yapakuliwa mara milioni 50 mpaka sasa

Je Apple kuachana na matoleo ya iPhone ya GB 16 ni habari nzuri?

Hili linategemea unaliangalia kwa mtazamo gani, kuna watumiaji wengi ambao wamekuwa wakilalamika kuona bado Apple wanaendelea kuleta matoleo ya iPhone ya GB 16 wakati kwa sasa uwepo wa apps nyingi na uhitaji wa kuwa na vitu kama muziki na video katika simu mwisho wake zinakuwa zinawahi kujaa sana – na pia iPhone hizi hazina sehemu ya kutumia memori kadi.

SOMA PIA:  Apps mbalimbali katika simu moja kwa akaunti mbilimbili

Kwa namna nyingine pia kuna uwezekano mkubwa Apple wakapandisha bei kidogo kwa toleo la chini la iPhone linalokuja…kwa kutumia kigezo cha kuwa kwa sasa zitakuwa na ujazo mkubwa zaidi.

iPhone 7 inakuja lini?

Inasemekana Apple wamejiandaa kuja kitofauti zaidi katika toleo la iPhone 7. Ushindani umekuwa mkubwa sana katika simu janja kwa sasa na ata wao mapato yao kutokana na mauzo ya simu za iPhone yameanza kushuka kwa mara ya kwanza na hivyo ni muhimu sana kuja na kitu kipya sana kitakachowavutia watu kubadilisha simu zao. iPhone 7 inategemewa kutambulishwa mwezi wa tisa mwaka huu.

SOMA PIA:  Kipengele cha 'Smart Battery' kwenye simu za Google Pixels

Endelea kutembelea TeknoKona na tutakupa taarifa za maendeleo ya ujio wa iPhone 7.

Vipi wewe una mtazamo gani juu ya suala la ukubwa wa diski uhifadhi (storage) katika simu? Kiasi gani kinatosha kwa matumizi yako?

Vyanzo: Slate.com na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com