fbpx

Apple kubadilisha baadhi ya betri katika iPhone 6S zinazojizima zenyewe

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Inaonekana si Samsung tuu waliokatika matatizo na suala la betri. Apple kubadilisha baadhi ya betri katika toleo la simu za iPhone 6S ambazo zimegundulika huwa zinajizima zenyewe.

apple kubadilisha baadhi ya betri

Tatizo hilo limeshafuatiliwa na kuonekana kutokea tayari kwa watumiaji kadhaa nchini China, Apple wenyewe wamesema tatizo hilo lipo kwa baadhi ya simu kadhaa ambazo tayari wamezitambua kwa namba zake (serial number), na simu hizo zilitengenezwa kati ya mwezi wa tisa na kumi mwaka jana.

Apple wamehakikishia watumiaji wake ya kwamba tatizo hilo ni la kikawaida na halina hatari yeyote kwa watumiaji: ‘hapa ni ukilinganisha na lile la Samsung Galaxy Note 7.

Tatizo la kujizima ghafla kwa simu za iPhone 6S umeonekana kwa baadhi ya simu hasa pale kiwango cha chaja kwenye simu hizo kikiwa kati ya asilimia 50 hadi 60.

INAYOHUSIANA  Uwezo wa kujua ujumbe umesambazwa mara ngapi kwenye WhatsApp

Mabadiliko hayo ya betri yatafanywa bure kabisa kwa wateja ambao simu zao zinatatizo hilo.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana na sisi kupitia FacebookTwitterInstagramYouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.