fbpx

Apple kufanyia matengenezo bidhaa zao bure

0
Sambaza

Ni nadra sana kwa kampuni kama Apple kutangaza kuwa itafanya matengenezo ya bidhaa fulani ambazo zimekwisha kununulika bila ya kuwatoza gharama yoyote wahusika lakini daima huwa kuna sababu maalum.

More about the author

Ulimwengu mzima unajua kuwa nchi ya Japan ilikumbwa na mafuriko mapema mwezi Julai 2018 hivyo katika taarifa rasmi yaliyoitoa Apple imesema itazifanyia matengenezo bila kudai malipo bidhaa zao za kidijitali (iPhone, iPad, Mac na iPod) zilizoharibika kutokana na mafuriko yaliyokuwa yameikumba nchi hiyo.

Ili Apple waweze kuifanyia matengenezo kifaa husika mwenye nacho itambidi athibitishe kuwa kifaa kilichoharibika ni cha kwake.

Mwenye mali hatohitajika kupeleka kifaa chake bali imetolewa namba maalum ambayo atapiga na mtu kutoka kampuni fulani ataipitia na kuipeleka kisha baada ya kutengenezwa atarudishiwa bila yeye kuifuata.

matengenezo

Bidhaa mbalimbali ambazo zinatengenezwa na Apple.

Mpango huo umepanga kuendelea mpaka mwisho wa mwezi Septemba 2018 bila ya kuongeza muda ingawa kwa baadhi ya maeneo wateja wanaweza wakachelewa kupata huduma kutokana na barabara kuharibika.

Vyanzo: The Verge, MacRumors

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Sasisho muhimu kwa Huawei Mate 20 Pro
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.