Apple Kuja Na Emoji Mpya Katika Vifaa Vya iOs na macOS!

0
Sambaza

Hii ni habari ya aina yake kwa watumiaji wa vifaa vya iOs, emoji mpya zipo njiani. Pengine ulikua hujui kama jana (17/07/2017) ndio ilikua siku ya Emoji Duniani!.

Apple imeonyesha baadhi ya Emoji ambazo zitatoka na kutumia katika vifaa vya iOs na macOS hata watchOS Mbeleni mwa mwaka huu.

Emoji Mpya Kwa Vifaa Vya iOS na macOS

Apple imesema ” Ni muhimu sana watu kuweza kujielezea wenyewe kwa kina zaidi, ongezeko la wanyama na viumbe vingine, sure mpya za smile na mengine mengi yatafanikisha hilo”

Emoji mpya ambazo zitaongezwa ni kama mwanamke ambae kavaa skafu kichwani , mwanaume mwenye mandevu, mwanamke anaenyinyesha, Emoji za vyakula kama vile nazi n.k

SOMA PIA:  Apps za wanyama zawekewa katazo kulinda usalama wa wnyama pori

Pia katika wanyama na viumbe kutakua na ongezeko, Pundamilia na zombi ni moja wapo ya ongezeko.  Kwa kifupi mambo yatakuwa ni mengi ya kukuburudisha wakati ukiwa katika mazungumzo.

Emoji Mpya Kwa Vifaa Vya iOS na macOS

kingine kizuri ni kwamba kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa series ya Game Of Thrones (GOT), mmoja kati ya mchezaji humo ametengenezewa emoji yake. Ndio! Khaleesi ambae ni mama wa ‘Gragon” atakuwa na Emoji yake.

SOMA PIA:  Unsane: Filamu iliyorekodiwa kwa kutumia iPhone 7

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment, hili wewe umelipokea vipi? je ulikua unajua kama siku ya Emoji duniani?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila SIku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com