Apple Kutengeneza Simu ya Kujikunja Ifikapo 2020, kushirikiana na LG!

Apple Kutengeneza Simu ya Kujikunja Ifikapo 2020, kushirikiana na LG!

0
Sambaza

Taarifa zilizotoka ni kwamba Apple wanawekeza majeshi yao katika kampuni ya LG ili kuhakikisha kuwa wanatengeneza simu ambazo zitakua ni vioo vya kukunjika.

source site

follow url Kumbuka katika iPhone X, Apple inategemea vioo vya OLED kutoka kwa Samsung ambae pia ni msambazaji pekee wa vioo hivyo kwa Apple.

Mkurugenzi wa Apple Bwana Tim Cook

Mkurugenzi wa Apple, Bwana Tim Cook

Teknolojia hii itaanza kufanyiwa kazi mara tuu ifikapo 2019 kwa sababu ndipo uzalishaji mkuu utakapoanza. Apple wanafanya kila njia ili na LG wawe wanawatengenezea vioo vya OLED na hii itasaidia kupunguza gharama za uzalishaji ukiangalia kwa sasa wanawategemea Samsung tuu ambao pia ndio washindani wao wa juu.

http://diasaonline.com/wp-content/uploads/photo-gallery/DSC02704.JPG Kwa sasa kampuni ya Samsung ndio inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi kuleta simu ya kujikunja mapema zaidi ya Apple. 

Lakini unaweza ukashangaa teknolojia hii kwa Samsung inaweza ukaja mwakani tuu na wakaachia simu janja ambayo inakunjika katika kioo chake cha OLED. Kwa Apple ni mpaka 2020 ifike na unaweza shangaa kuwa simu zinaanza uzwa rasmi mwaka 2021.

INAYOHUSIANA  Msichana anusurika kifo kwa sababu ya 'Selfie'

Vile vile hapo mwanzoni zilitoka taarifa kuwa Apple ina mpango wa kutumia vioo kutoka Japan (Ambavyo vinapinda) katika simu zake zijazo.

Apple Kutengeneza Simu ya Kujikunja Vioo Vyenye Umbo La Kupinda Kutoka Japan Ambavyo Pia Apple Wana Mpango Navyo

Apple Kutengeneza Simu ya Kujikunja: Vioo Vyenye Umbo La Kupinda Kutoka Japan

LG wako mbioni kufungua kiwanda chao ambacho kitatumika katika kutengeneza vioo hvyo vya OLED na inasemekana kuwa Apple itachangia kiasi cha dola bilioni 2.6 kama sehemu ya uwekezaji.

Pata picha simu kama hii inaweza ikauzwa bei gani? Ningependa kusikia kutoka kwako je unahisi simu ambayo ina kioo cha kukunjika itakuaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.