fbpx

Apple na Oprah kufanya kazi kwa pamoja

1
Sambaza

Katika wanawake watano waliotokea kwenye maisha ya chini sana na kupambana mpaka kuwa moja ya watu mashuhuri lakini pia tajiri duniani huwezi kuacha kutaja jina la Bi. Oprah Winfrey.

Bi. Oprah ambae kwwa miaka mingi tu alikuwa akiendesha kipindi chake mwenyewe, The Oprah Winfrey Show na kuacha kurusha kipindi hicho miaka kadhaa iliyopita sasa Apple wameamua kukaa chini na mwanamama huyo ili watengeneze vipindi.

Katika kila kitu ni muhimu kufanya ukiwa umejidhatiti kwani Apple anapata upinzani mkali kutoka kwa Netflix, Amazon ambao wote hao wanafanya huduma kuangalia vitu mtandaoni (online streaming).

Apple na Oprah kufanya kazi

Bi. Oprah anafahamika kwa kuweza kuwaunganisha watazamaji kutokana na yale maneno yake kulingana na mjadala wa siku husika.

Hatua ya Apple kufanya kazi na Bi. Oprah itawaongezea wapenzi na wateja wapya na hivyo kutanua wigo wa watazamaji kwenye masuala ya kuangalia vitu mtandaoni papo hapo. Utakumbuka Netflix walitangaza kuwa watakuwa wakifanya vipindi na rais mstaafu Obama pamoja na mkewe.

INAYOHUSIANA  Kupanda kodi kwa baadhi ya makampuni

Visit Your URL Bi. Winfrey ni mwanamama aliyewapa nguvu kwa maneno yake, msaada wa hapa na pale mabinti, wanawake, wake kwa waume na watu mbalimbali duniani na kuamini kuwa hakuna kinachoshindikana chini ya Jua.

Apple hawajaweka kiasi ambacho wamemlipa Bi. Oprah kuweza kufanya nao kazi kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini inaaminika kuwa ni kiasi kikubwa sana.

Vyanzo: Apple Newsroom, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|