Apple Na Samsung Watupwa Mbali: Huawei Imeongoza Mauzo China Katika Robo Ya Pili Ya 2016! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple Na Samsung Watupwa Mbali: Huawei Imeongoza Mauzo China Katika Robo Ya Pili Ya 2016!

0
Sambaza

Yaani ukiachana na simu janja zote katika soko la simu nchini china kampuni ya Huawei ndio inashika namba moja katika mauzo.

buy robaxin
Huawei imeyatupa mbali makampuni mengine kama vile Apple ambao wameshika namba tano na wapinzani wao wengine, Samsung ambao hawajashika hata tano bora.

Baadhi Ya Simu Za Huawei

cheapest place to buy topamax Baadhi Ya Simu Za Huawei

go site Taarifa hizi zimetolewa na mtandao wa IDC. Katika repoti ambayo mtandao huo ulitoa ni kwamba huawei ilisafirisha simu milioni 19.1 mpaka mwezi wa 6 mwaka 2016. Na hiyo ni 15.2 % ya ongezeko la namba ya simu zilizouzwa na kampuni hiyo katika kipindi cha nyuma.

Kwa sasa kampuni ya Huawei ndio imeshikilia namba moja huku ikifuatiwa na OPPO na Vivo (wote hawa wanajihushisha na simu janja pia).

INAYOHUSIANA  Apple kufanyia matengenezo bidhaa zao bure

Kwa upande wa Xiaomi soko limeshuka kwani waliuza simu milioni 10.5 wakati msimu uliopita ndio walishikilia usukani kama vinara (namba moja) kwa kuuza simu milioni 17.1 katika msimu uliopita.

Apple na wenyewe ni majanga (lakini inafahamika kuwa nchini China huwa wafanyi vizuri licha ya simu zao kuwa bei ghali) wameuza simu milioni 8.6 na hiyo namba imeshuka kwani awali waliuza simu nyingi zaidi ya hizo.

Ripoti Hiyo Ya IDC

Ripoti Hiyo Ya IDC

Hata hivyo kampuni ya Xiaomi imepingana na ripoti hiyo na kuomba kuwa kampuni lingine liweze kusimamia upya ripoti hiyo kwani ina makosa. Wao Xiaomi wanasema kuwa waliuza simu milioni14.2, japokuwa katika repoti ya IDC bado hata ukichukua hiyo namba bado Xiaomi wanakuwa katika nafasi ya nne. Lakini bado Xiaomi hawaamini kwani kama wameweza kukosea kwao, wanaweza wakakosea na kwingine – Xiaomi wakisema hivyo.

INAYOHUSIANA  Huawei na simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Apple kwa upande mwingine mauzo yake yanazidi kushuka sana katika soko la china, kumbuka hata simu yake ya iPhone 5se haikufanya vizuri sana kwani watu wengi walihitaji simu zenye vioo vikubwa.

Muonekano Wa Simu Mojawapo Ya Xiomi Na Ile Ya Vivo

Muonekano Wa Simu Mojawapo Ya Vivo Na Ile Ya Xiaomi

Cha muhimu kuzingatia hapa ni kwamba taarifa hizi ni mauzo ya robo ya pili ya mwaka 2016 kwa mauzo ya soko la simu huko nchini china.

Je kwa mtazamo wako unahisi hii ripoti iko sahahi, Yaani hata Samsung hawapo katika tano bora? Hebu niandikie hapo chini sehemu ya comment, ningependa kusikia kutoka kwako.

Tembelea Teknokona kila siku ili kuwa karibu na teknolojia. Kumbuka TeknoKona Diama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.