APPLE watambulisha iPhone 8 na simu ya iPhone X ya zaidi ya Tsh Milioni 2

0
Sambaza

Apple watambulisha iPhone 8 na simu nyingine waliyoipa jina la iPhone X inayowakilisha kushangilia kwao kwa miaka 10 ya simu za iPhone.

Simu ya iPhone X imeleta mageuzi kadhaa, ni simu ya kwanza kutoka Apple iliyoingia kwenye kundi la teknolojia inayopendwa sana kwa sasa na Samsung ya kuweka display/kioo eneo kubwa la simu nzima.

Sifa za iPhone X, iPhone 8 na 8 Plus

simu ya iPhone X iPhone 8 na 8 Plus

Muonekano wa iPhone X iPhone 8 na 8 Plus

iPhone X inatumia display inayofika hadi kwenye kona zote pembeni mwa simu hii. Display ni ya teknolojia ya OLED na ni ya ukubwa wa inch 5.8

Muonekano mzima wa iPhone 8 ni kama wa iPhone 7 ila tofauti kubwa ni kwamba imezungukwa na ‘body’ ya kioo (glass).

Kuna teknolojia zingine mbalimbali zilizozoeleka kama vile waterproof zimeendelea kuwekwa.

 

SOMA PIA:  Samsung yaendelea kuvunja rekodi za faida. Ijue biashara iliyowapa faida.

> iPhone X yaachana na Home Button

Hakuna ‘home button’, scheme maarufu ya iPhone inayomrudisha mtumiaji eneo la nyumbani la display.

> Face ID

Inaweza kuondoa ‘lock’ ya sim kwa kutambua sura ya mtumiaji – wameiita teknolojia ya Face ID. Unaweza sema teknolojia hii ishakuwepo muda mrefu ila tifarti kuu ni kwamba kwa iPhone X itatumia teknolojia za sensor na si kamera pekee katika utambuzi wake na hivyo kuwa bora zaidi.

Face ID itakuwa kwenye iPhone X na itatumika badala ya teknolojia ya Touch ID.

‘Kwa wengi wanaona hapa hakuna jipya, wewe unaonaje?’

> Chaji bila kutumia waya!

Simu zote zinaweza kuchajiwa kwa njia za bila waya kutumika – ‘wireless charging’. Teknolojia hii ishakuwa maarufu kwa makampuni mengi ya simu za Android.

SOMA PIA:  Nile X: Simu janja ya kwanza kutengenezwa Misri yazinduliwa

> Kuchaji kwa baraka zaidi

Simu zote zinakuja na teknolojia ya ‘fast charging’, hii inamaanisha zinauwezo wa kupata chaji nyingi kwa haraka ndani ya muda mfupi. Simu zote zinauwezo wa kufikia kiwango cha chajá cha asilimia 50 ndani ya nusu saa.

Apple wamedai betri la toleo la iPhone X litadumu na chaji masaa mawili zaidi ukilinganisha na iPhone 8 na 8 Plus.

> Kamera

Zote zinakuja na kamera za Megapixel 12, hij ni kwa iPhone 8 na 8 Plus pia. Kamera zote zinakuja na teknolojia bora za kuhakikisha ubora mkubwa wa picha. iPhone X na iPhone 8 Plus. Utaweza rekodi video za HD

Kwa kamera ya selfi zinakuja na kamera ya megapixel 7, flash na uwezo wa kurekodi video za HD za kiwango cha 1080p HD.

iphone emoji

Apple wameboresha pia emoji zake na pia kuzipa simu zake uwezo wa kutengeneza emoji kulingana na muonekano wa mtumiaji wa simu husika. Hii ni kwa kutumia kamera.

emoji iphone kamera

Kupitia kamera yake iPhone itaweza kumpatia mtumiaji emoji ya kutumia kulingana na muonekano wa sura mtumiaji atauweka

> RAM

SOMA PIA:  Kipengele cha "Private Reply" kiliwekwa kimakosa (kutoka kabla ya muda wake)

Apple huwa hawaweki wazi Ila tayari watafiti wanaamini iPhone X na iPhone 8 Plus zinakuja na RAM ya GB 3 wakati toleo la iPhone 8 lina RAM ya GB 2.

> LTE na Bluetooth

Pia zinakuja na uwezo wa teknolojia ya mawasiliano ya LTE Advanced na toleo la Bluetooth 5.0.

> Bei

Simu ya iPhone X itapatikana kwa bei ya $999 (Zaidi ya Tsh Milioni 2.2) kwa toleo la GB 64 na $1,149 (Takribani Tsh Milioni 2.56) kwa toleo la GB 256. iPhone 8 inaanzia kwa bei ya  $699 ambayo ni takribani Tsh  Milioni 1.56, iPhone 8 Plus inaanzia $799 ambayo ni takribani Tsh Milioni 1.759.

Simu hizi zinaanza kupatikana kuanzia Novemba 3 mwaka huu. Watu wamezipokea kwa mitazamo tofauti, bei ya iPhone X imetumiwa kiutani hadi kulinganisha na bei ya figo ya binadamu 🙂 . Je wewe umezipokeaje?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com