Kwa Ufupi! Kwa mara ya Kwanza kabisa, Apple walitambulisha Apple Tv (Kwa kipindi hicho waliita iTV) mwaka 2006. Ilikusudiwa kushusha media mbalimbali mtandaoni, kupitia iTunes ya kompyuta na kuchezwa katika TV yako.
Septemba 2010, Apple walitambulisha Toleo la pili la Apple TV. Safari hii, haikuwa kubwa sana na ikiwa na mfumo endeshaji wa iOS na sasa haikuwa inapakua kutoka iTune, bali ilikua inacheza moja kwa moja (Streaming).
Mwaka 2012, Apple walitambulisha Toleo liliyopo sokoni kwa sasa, Apple TV-Toleo la tatu ambalo linacheza video kwa kiwango cha 720p.
Apple-TV ni kicheza media kinachopakua media zinazopatikana mtandaoni na kuzicheza katika TV yako. Apple TV hushusha data za kidigitali kutoka mtandaoni kutoka katika vyanzo mbalimbali na kuvicheza katika Televisheni.
Kwa lugha nyepesi, Apple TV inafanya kazi kama ving’amuzi vyetu vya kawaida – tofauti kubwa ikiwa ni yenyewe inapakua data zake kutoka Mtandaoni moja kwa moja.
Ni kifaa kinachotumia HDMI, ambapo ili kutumika kinahitaji kuunganishwa katika TV yenye uwezo wa kupokea mawimbi ya (High Definition) yanayounganishwa kupitia waya wa HDMI.
Apple TV inacheza data zake kutoka vyanzo vingi tofauti, kama Netflix, iTunes Store, Hulu Plus, Now TV(Uingereza Pekee), Youtube Live, Vevo, pamoja na baadhi ya wasambazaji wa TV kupitia cable zinazofanya kazi pamoja na Apple TV.
Ni moja ya vifaa vya kisasa zaidi vya burudani, hasa katika ulimwengu huu uliokithiri katika matumizi ya teknolojia thabiti. Kwa sasa, Apple TV wanajiandaa kuachia toleo jipya la Apple TV, ambalo tayari limezua gumzo kubwa mtandaoni kutokana na vilivyomo katika kifaa hicho kipya.
Inatazamiwa kuachiliwa Septemba mwaka huu, toleo jipya linategemewa kuwa na vitu vifuatavyo;
- SIRI inayokupa uwezo wa kutafuta chochote mtandaoni kupitia sauti yako
- App Store ya Apple
- Remote ya kugusa, kwa ajili ya vitufe vya ziada kama vile sauti, bluetooth na matumizi ya hewani (Utaweza kuchora herufi hewani, na apple TV itatambua ni herufi gani, kama Wii inavyofanya kazi) na mengine mengi.
- Kufanya kazi na vifaa vingine kwa ajili ya magemu makali zaidi kutoka Apple
Hivyo basi, Unaweza kufanya nini ukiwa na Apple TV?
- Kuangalia Video (Streaming) moja kwa moja
Hapa utaweza kuangalia kutoka vyanzo tofauti kama Netflix, Hulu, HBO GO/HBO NOW, ESPN, PBS, YouTube, n.k
- Kusikiliza Audio moja kwa moja.
Hapa utaitumia kama unavyotumia iTunes katika kompyuta au simu yako.
- Kucheza Games
- Kutumia App kali za Apple Store
- Kucheza audio zilizopo katika iPhone au iPad yako.
- Kukiangaza kifaa chako cha iOS katika TV
Hapa utaweza kuunganisha iPhone au iPad yako na apple TV, kisha ukawa unatumia kioo cha TV kuperuzi simu yako
Bado kuna vitu hujavijua kuhusu AppleTv? Usisite, wasiliana nasi kupitia Comments, na tutajibu maswali yako moja kwa moja kuhusu Apple TV.
Vyanzo : iMore, Wikipedia na CNet